Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Songea
ZAIDI ya wateja 380,000 wakiwemo watumishi wa Serikali, wafanyabiashara, wanafunzi na wajasiriamali wamejiunga na huduma ya CRDB Al Barakh ambayo inatoa fursa kwa watu kupata huduma kuendana na imani zao hapa nchini.
Akizungumza kwenye hafla ya kufuturisha wateja na wadau wa benki hiyo iliyofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Chandamali uliopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma jana mkurugenzi wa wateja wakubwa wa benki hiyo Mussa Kitambi alisema kuwa huduma za Al Barakh zimefuata misingi ya sheria.
Alisema kuwa huduma hizo zinapatikana katika matawi yote nchini mpaka sasa wameweza kutoa uwezeshwaji wa zaidi ya shilingi bilioni 172 na kwamba wanajivunia ubunifu huo ambao umekuwa na mwitikio mkubwa wa wateja.

“Tunapoendelea na funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ninawiwa kukawakaribisha kuendelea kutumia huduma zetu za Al Barakh zinazofuata misingi ya sheria, wateja wetu wanaweza kutunza amana zao na kufanya miamala kupitia akaunti maalumu za Al Barakh iwe ni kwa wanafunzi,wafanyakazi, wafanyabiashara au wajasiliamali ambapo wanaunganishwa na kadi maalumu za Al Barakh. ” alisema Kitambi.
Awali akizungumza kwenye afla hiyo meneja wa CRDB kanda ya kusini Denis Mwoleka alisema kuwa benki ya CRDB imekuwa na utaratibu na utamaduni wa kuandaa futari kwa ajili ya wateja na wadau wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani wakiamini kuwa funga ya Ramadhani ni shule ya mafunzo ya maadili mema, upendo na mshikamano.
“Napenda nichukuwe fursa hii kuwashukuru sana kwa sapoti mnayotupatia benki yetu ya CRDB kupitia dirisha letu tunaloliita Al Barakh benki kwa kweli tunashukuru sana tumefungua akaunti nyingi lakini tumefanya biashara nyingi kupitia biashara yetu ya Al Barakh na naamini kabisa kwamba tunapoenda kuanza kujiandaa na imani hii basi mnafahamu kuwa kuna dirisha zuri ambalo lipo ndani ya CRDB linalowawezesha kufanya huduma ” alisema Mwoleka .

Kwa upande wake shekhei mkuu wa Mkoa Ramadhani Mwakilima alisema kuwa dirisha hilo la Al Barakh limesimamiwa kwa ukamalifu na baraza kuu la uisilamu la Tanzania Bakatwa chini ya mufti na shekhar mkuu wa Tanzania Abubakar Zuberi na ukienda kwenye ofisi ya shekhar wa Mkoa yeyote Tanzania utakuta kuna walaka Maalum unaomtaka huyo shekhar kuhakikisha anasimama na kuisimamia Al Barakh katika Mkoa wake.
” Mgeni rasmi ni kama kusema CRDB Al Barakh na Bakwata ni mume na mke ambao kwa namna yeyote iwezekanavyo ahuwezi kututenganisha kwa hiyo banki ya CRDB wakati mmewaza kufanya hili jambo hamkukosea na ndio Islamic banki ya aina yake kuanzishwa ikilinganishwa na zilizowahi kupita kwenye aina nyingine za benki Tanzania. “Alisema shekhar Mwakilima.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile ambaye alimwakilisha mgeni rasmi mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas alisema kuwa utaaratibu wa benki ya CRDB wa kuandaa futari hiyo maalumu kwa wateja na wadau wao katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ni jambo jema kwani linaleta mshikamano baina ya wateja na watumishi wa benki hiyo.


