Na Tatu Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) CPA Anthony Kasore ametoa wito kwa jamii kuacha kuwafungia watu wenye mahitaji Maalum na badala yake wawapeleke VETA kupata ujuzi wa aina mbalimbali.

Aidha amesema kuwa Serikali ya Chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imevutia wawekezaji wengi ambapo nguvu kazi hiyo Uwekezaji itatoka VETA.

CPA Kasore ameyasema hayo wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.amesema kuwa katika maonesho hayo kuna Ubunifu wa Teknolojia mbalimbali ambazo zinakwenda kutatua changamoto katika sekta zote za kiuchumi.

“Kwa kutambua changamoto ya makundi Maalum, sisi kama VETA tunatoa wito wa jamii kuacha kuwafungia ndani kwani kufanya hivyo ni kuwakosesha fursa za msingi kwa kundi hilo.

“Sisi tunataka vijana wote nchini wapate ujuzi ambao unakwenda kuwa fursa yao katika kuendesha maisha yao kutokana kuwepo kwa mahitaji mengi ya ujuzi huo kutumika,” amesema CPA Kasore.

Amesema kuwa baada ya kutambua kuwa kuna uwekezaji mkubwa wa viwanda wameanzisha fani ya Mechatronics ambapo wanaosomea kozi hiyo watakwenda huko kutokana na mitambo ya viwanda kuhitaji wataalam hao.

Ameongeza kuwa wanakwenda na Sera ya Serikali ya kuwa wanafunzi wote wanafika kidato cha nne ambapo watapata kusoma mafunzo ya ujuzi hapo ndipo VETA kuwa na kutengeneza Walimu watakwenda kuwafundisha ujuzi.

CPA Kasore amesema kuwa vijana wa Tanzania katika maeneo yote vyuo vya VETA vimejengwa waende kupata mafunzo ya ujuzi ambapo watakuwa wameondokana na tatizo la ajira kutokana na fursa zilizopo katika maeneo yao.

Amesema katika kuwa Kilimo ni Uti wa mgongo ambapo wanaotaka kufanya Kilimo watapata mafunzo na ujuzi na Kilimo cha uhakika na sio Kilimo cha kubahatishaa hali kadhalika kwa Sekta mifugo na Uvuvi wafanya hivyo hivyo.

Aidha amesema kuwa serikali imeendelea kuwekeza Ujenzi wa vyuo kuanzia Wilaya hadi Mikoa ikiwa na lengo ya kutoacha nyuma watu wote kwenye kupata mafunzo ya ujuzi.

CPA Kasore amesema kuwa Hadi wastaafu wanaweza kupata mafunzo ya ujuzi na kuweza kuendelea kuzalisha bila kutegemea mafao ya ustaafu.

Please follow and like us:
Pin Share