Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma.

TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)imewataka watanzania kutumia bunifu zinazoibuliwa na vijana kwa lengo la kutoa hamasa na kuziendeleza hali itakayosaidia kutatua baadhi ya kero kwenye jamii .

Mkurugenzi Mkuu (COSTECH) Dk.Amos Nungu, amesema hayo  jijini hapa  wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yanayofanyika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

“Kwa sasa serikali kupitia COSTECH imeweza kuwaweka sokoni vijana wengi ambao wameonekana kuwa wabunifu kwa kuwapatia vibali vya kuwaendeleza na kuwajengea uwezo wa kiuchuni jambo ambalo linaendelea kutoa hamasa katika jamii”alisema

Amefafanua  kuwa Vijana wengi ambao wanajitokeza kwa kujitambulisha kuhusu ubunifu walionao wamekuwa wakisaidiwa kwa kuendelezwa au kuunganishwa katika mashirika mbalimbali nchini.

“Vijana acheni  kukopi bunifu za wengine na kubuni kitu  cha utofauti ili muweze kuweka rekodi ya kipekee kama vijana kwa kuwa wa kwanza kubuni bunifu za kipekee na zenye tija na kuleta ushawishi kwenye jamii,”amesema.

Dk.Nungu amewataka watanzania kuziamini na kuzitumia bunifu zinabuniwa na vijana wa kitanzania ikiwemo kuzinunua na kurejesha mrejesho kwa wabunifu kama sehemu ya kuziboresha.

Please follow and like us:
Pin Share