Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo inasema inajitahidi kuepusha mauaji mjini Goma, lakini haitaachia eneo lolote baada ya waasi wa M23 kudai kwamba wameuteka mji huo.
Katika taarifa kwenye mtandao wa X, Waziri wa Mawasiliano Patrick Muyaya aliwataka watu kusalia majumbani kwa usalama wao.
Pia aliwataka watu kujiepusha na uhalifu au uporaji, na kupuuza propaganda za Rwanda.
Muyaya pia alirudia kauli za awali zinazodai kuwa wanajeshi wa Rwanda wako ndani ya DRC na wanashirikiana na waasi wa M23 katika mapigano yanayoendelea mjini Goma.
“Sisi sote ni walinzi wa eneo letu,” Muyaya alisema, akiongeza kuwa “hakuna eneo lolote litatolewa”.