MKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi (PPP) Davidi Kafulila, kwa kuendeleza zoezi la kuibua miradi katika maeneo mbalimbali nchini.
Chongolo ametoa pongezi hizo ofisini kwake alipotembelewa na timu ya mafunzo na uibuaji wa miradi kutoka kituo cha ubia, iliyofika kwa lengo la kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa huyo kujadili mambo yanayohusu miradi ya PPP.
Katika mazungumzo hayo, wawezeshaji hao kutoka kituo cha ubia, wamemjulisha Chongolo hali ya zoezi katika Wilaya zote tano zilizopo katika Mkoa wa Songwe.
Pia, Chongolo ameonesha umuhimu wa uwepo wa miradi ya ubia kwa Mkoa wa Songwe, ambao ni lango kuu kwa nchi za SADC, huku akisisitiza kuwa kuwepo kwa zoezi kutaleta mazoezi katika Mkoa huo.
![](https://www.jamhurimedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/1002512197.jpg)
![](https://www.jamhurimedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/1002512195.jpg)
![](https://www.jamhurimedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/1002512196.jpg)