MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga raia wa Zambia, Obrey Chirwa rasmi amesaini mkataba na Klabu ya Nogoom El Mostakbal Football Club ya nchini Misri.
Mshambuliaji huyo amejiunga na timu hiyo baada ya mkataba wake wa miaka miwili ya kuendelea kuichezea Yanga kumalizika kabla ya kutimkia Misri.
Mzambia huyo baada ya mkataba wake kumalizika aliuomba uongozi wa timu huyo kuondoka kwenye klabu hiyo na kwenda kutafuta changamoto nyingine kwingine na kumruhusu na klabu ya Ismailia ya nchini huko ndiyo alikuwa anaitaja.
Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo, Chirwa rasmi amesaini mkataba na kutambulishwa rasmi huku akikabidhiwa jezi ya klabu hiyo.
Hivyo, Chirwa kwenye msimu ujao ataitumikia Noogom El Mostakbal inayoshiriki Daraja la Pili baada ya kufikia muafaka mzuri na kusaini mkataba.