Wakati tu Malkia amefariki dunia, kiti cha enzi kinapitishwa mara moja bila sherehe yoyote kwa mrithi, Charles, Mkuu wa zamani wa Wales.
Lakini kuna hatua kadhaa za kiutendaji – na za kitamaduni ambazo lazima azipitie ili kutawazwa kuwa Mfalme.
Moja kati ya vitu vya kwanza atakavyofanya ni kuamua kama atatawala kama Mfalme Charles III, au kuchukua jina lingine.
Kwa mfano, jina la babu yake George VI lilikuwa Albert, lakini alitawala kwa kutumia mojawapo ya majina yake ya kati.
Charles anaweza kuchagua kutoka kwa mojawapo ya majina yake manne – Charles Philip Arthur George.Sio yeye pekee ambaye anakabiliwa na kubadilisha jina lake.
Ingawa yeye ndiye mrithi wa kiti cha enzi, Prince William hatakuwa Mkuu wa Wales moja kwa moja.
Hata hivyo, moja kwa moja anarithi jina lingine la baba yake, Duke of Cornwall.Mkewe Catherine atajulikana kama Duchess of Cornwall.
Pia kutakuwa na jina jipya la mke wa Charles, ambaye majina yake kamili yatakuwa Malkia Consort – neno linalotumiwa kwa mwenzi wa mfalme.
Katika muda wa saa 24 au zaidi baada ya kifo cha mamake, Charles atatangazwa rasmi kuwa Mfalme.
Hii itafanyika katika kasri la St James’s huko London, mbele ya baraza la sherehe linalojulikana kama Baraza la kukabidhi Mamlaka.
Hii inaundwa na wajumbe wa Baraza la Siri – kikundi cha Wabunge wakuu, wa zamani na wa sasa, na wenzao – pamoja na baadhi ya watumishi waandamizi wa serikali, makamishna wakuu wa Jumuiya ya Madola,na Meya wa London.
Zaidi ya watu 700 wana haki ya kuhudhuria, lakini kutokana na ilani hiyo fupi, huenda idadi halisi ikawa ndogo sana.
Katika Baraza la kukabidhi Mamlaka mnamo 1952, karibu watu 200 walihudhuria.Kiutamaduni, Mfalme hahudhurii.
Katika mkutano huo, kifo cha Malkia Elizabeth kitatangazwa na Rais wa Baraza la Siri (kwa sasa akiwa ni Penny Mordaunt Mbunge), na tangazo litasomwa kwa sauti.
Maneno ya tangazo hilo yanaweza kubadilika, lakini kiutamaduni imekuwa mfululizo wa sala na ahadi, kumpongeza mfalme aliyetangulia na kuahidi kumuunga mkono mfalme mpya.
Tangazo hili kisha linatiwa saini na watu kadhaa wakuu akiwemo waziri mkuu, Askofu Mkuu wa Canterbury, na Bwana Chansela.
Kama ilivyo kwa sherehe hizi zote,tahadhari itakuwa kwa kile ambacho kinaweza kuwa kimebadilishwa, kuongezwa au kusasishwa, kama ishara ya enzi mpya.
Baraza la kukabidhi Mamlaka hukutana tena kwa kawaida siku moja baadaye – na wakati huu, Mfalme atahudhuria, pamoja na Baraza la Siri.
Hakuna ”Kuapishwa” mwanzoni mwa utawala wa mfalme wa Uingereza, kwa mtindo wa wakuu wengine wa nchi, kama vile Rais wa Marekani.
Lakini kuna tamko lililotolewa na Mfalme mpya na kulingana na mila ya mwanzoni mwa Karne ya 18 atakula kiapo cha kuhifadhi Kanisa la Scotland.
Baada ya mbwembwe za wapiga tarumbeta,tangazo la umma litatangazwa kumtangaza Charles kama Mfalme mpya.
Hii itafanywa kwenye roshani juu ya Mahakama ya Friary katika eneo la Kifalme la St James, na afisa anayejulikana kama Garter King of Arms.
`Atasema: ”Mungu mwokoe Mfalme”, na kwa mara ya kwanza tangu 1952, wimbo wa taifa utakapopigwa maneno yatakuwa ”Mungu Mwokoe Mfalme”.
Risasi zitapigwa katika eneo la Hyde Park, Mnara wa London na kutoka kwa meli za wanajeshi wa majini, na tangazo la kumtangaza Charles kama Mfalme litasomwa huko Edinburgh, Cardiff na Belfast.
Ishara ya juu ya kukabidhi mamlaka itakuwa kutawazwa, wakati Charles atavikwa taji rasmi.
Kwa sababu ya maandalizi yanayohitajika, kutawazwa hakuwezi kutokea mara tu baada ya Charles kukabidhiwa madaraka – Malkia Elizabeth alirithi kiti cha enzi mnamo Februari 1952, lakini hakutawazwa hadi Juni 1953.
Kwa miaka 900 iliyopita kutawazwa kumefanyika Westminster Abbey – William the Conqueror alikuwa mfalme wa kwanza kutawazwa huko, na Charles atakuwa wa 40.
Ni huduma ya kidini ya Kianglikana, inayofanywa na Askofu Mkuu wa Canterbury.
Katika kilele cha sherehe hiyo, ataweka Taji la St Edward juu ya kichwa cha Charles – taji thabiti la dhahabu, lililoanzia 1661. Hiki ndicho kitovu cha Vito vya Taji kwenye Mnara wa London, na kwa sasa huvaliwa tu na mfalme wakati wa kutawazwa kwenyewe (kwa sababu lina uzito mkubwa wa 2.23kg).
Tofauti na harusi za kifalme, kutawazwa ni tukio rasmi la serikali – serikali inalipa, na hatimaye huamua orodha ya wageni.
Royal Family on Balcony at Buckingham Palace, London, pictured after Coronation, 2nd June 1953.
Kutakuwa na muziki, usomaji na ibada ya kumtia mafuta mfalme mpya, kwa kutumia mafuta ya machungwa, waridi, mdalasini, miski na ambari.
Mfalme mpya atakula kiapo cha kutawazwa mbele ya ulimwengu watu wakiwa wanatazama.
Wakati wa sherehe hii, atapokea taji umbo la duara na fimbo kama ishara ya jukumu lake jipya na Askofu Mkuu wa Canterbury ataweka taji imara la dhahabu juu ya kichwa chake.
Makala haya kwa msaaada wa BBC