Na Dotto Kwilasa,JamhuriMedia,Dodoma

Rais wa Chama Cha Mawakili wa Serikali Tanzania Deus Shayo amesema Chama hicho kinatarajia kufanya Mkutano wake Mkuu Aprili 14 hadi 15 mwaka huu Jijini Dodoma huku akiwataja zaidi ya Wanachama 2000 kuwa wanaweza kushiriki mkutano huo.

Ameeleza hayi leo Aprili 12,2025 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari
na kueleza kuwa Naibu Waziri Mkuu,Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo.

Rais huyo amesema mkutano huo utakuwa ni jukwaa la Mawakili kupata fursa ya kujaliana mambo ya kitaaluma na changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta hiyo.

Licha ya hayo ameeleza kwa Wanachama wa Chama hicho ni Mawakili na wanasheria wanaotoka kwenye taasisi za umma ambapo amedai kutakuwa na jukwaa la kitaaluma kujadili maslahi na maendeleo ya sekta ya Sheria na maadili kwenye Utumishi wa Umma.

Amesema hiyo itakuwa ni fursa na sehemu ya mafunzo kwa mawakili hao ambapo watajengeana uwezo.

Kutokana na hayo ametoa rai kwa Waajiri wote kuwaruhusu wafanyakazi wao na kuwawezesha kushiriki Mkutano na kueleza kuwa ushiriki huo ni muhimu kwa tathmini na mwelekeo kama walinzi wa uchumi.