Na Ruja Masewa, JamhuriMedia, Kyela

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Kyela, kimenyimwa mkutano wa No Reform, No election kisa kikiwa ni vurugu za viongozi miongoni mwao .

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama hicho wilayani Kyela Victoria Swebe, kutangaza kuwasimamisha viongozi sita akiwemo Katibu wa chama wilayani humo Job Mwakabanje, huku Donald Elukaga Mwaisango akifutiwa uanachama.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kufuatia kuikosa fursa ya mkutano huo, Wachama na viongozi wenye hasira wa Kata na Vijiji, wamemshutumu mwenyekiti Swebe kwa kuendeleza makundi na kutaka kuvuruga nguvu ya chama hicho wilayani Kyela na kuhoji, kwa nini yeye peke yake akosane na watu sita? Atakuwa ana matatizo!!

Viongozi waliosimamishwa ni Elukanga Mwaisango, Timothy Mwaluvanda, Abeid Mwambogoja, Ashura Mwanjala na Prosper mwakilembe, huku

“Wananchi wilayani Kyela wana kero nyingi wanazofanyiwa na baadhi ya viongozi wa Serikali ambao ni miungu watu, wanazuia mikutano ya vijiji, ukiwemo uhuru wa kuabudu na makanisa kufungwa. Je, kwa nini hawawi msaada wa kutatua kero hizo?.alihoji Dickson Mwanjala.

Mchungaji Maka Mwakyusa wa Kanisa la Kiinjilili la Kilutheri la Afrika Mashariki (KKAM) Kata ya Ipinda alishauri akidai, kama Watu wanazuiwa kuabudu, wakakosa fursa ya ELIMU ya kusikiliza hata mikutano ya siasa, tusishangae wakiuana na kuwa Wezi, Majambazi na kuwa Wachawi.

Nje ya Mkutano wa ndani, nmoja wa Wanachama wa Chadema wa Matema uliofanywa na Makamu Mwenyekiti John Heche aliyeomba asitajwe alidai,

Uongozi wa Juu Kyela una matatizo. Ulipoingia madarakani ulikuwa na viongozi mfukoni mwao, lakini uchaguzi ulipofanyika ulikuja tofauti, hivyo ukichanganya na makundi ya timu Mbowe na Lissu, ndiyo yanaiwatesa timu Lissu wasiwafanyie kazi wananchi.

“Ikiwa hata wakiwa msibaniwanaonyesha ukubwa na protocal, hayo ni wapi na wapi? Hiyo ni aibu kwa kiongozi.
Utashangaa, anapoambiwa kaa na katibu wako, utasikia yeye anadai, “mimi sina katibu ni uongozi gani huo wa pamoja team management?”.alisema.


Aidha wanachama kyela wamemtaka Katibu aliyeshindwa kinyang’anyilo cha Uongozi asiwe chawa wa Mwenyekiti Victoria ili kukivuruga chama wilayani humo ambacho wamedai kimejengwa kwa gharama kubwa.

Hata hivyo Wanachama hao wameushauri uongozi wa kitaifa wakidai, kama suluhu itafanyika na halafu tabia hiyo ya kuingiliana madarakani kati ya Mwenyekiti Victoria na Katibu Mwakabanje itaendelea, uongozi wa Taifa uchukue hatua kali, na ikishindikana wao watawataka wawapishe ili kukinusuru Chama.