Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
Dar es Salaam

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeonesha msimamo wake wa kutorudi nyuma licha ya vizingiti vinavyowekwa dhidi ya wanachama wake, ikiwemo kuzuiwa kwa baadhi yao kuhudhuria kesi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu lissu

Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 25,2025 katika makao makuu ya CHADEMA, jijini Dar es Salaam, akamu Mwenyekiti CHADEMA , John Heche, amesema chama hicho kiko tayari kulipa gharama yoyote kwa ajili ya kusimamia haki, ikiwa ni pamoja na maisha yao.

“Hatuwezi kukubali kuzuiwa kwenda kusikiliza kesi ya mwenyekiti wetu. Tutaendelea kwenda na tuko tayari kufa kwa ajili ya haki. Kama chama, hatutarudi nyuma,” amesema Heche.

Aidha, Heche ameeleza kuwa ifikapo Aprili 28 2025, CHADEMA itakuwa na mawakili wapya wa kimataifa kwa ajili ya kuimarisha utetezi wa mwenyekiti wao. Kwa sasa, mawakili wa haki za binadamu tayari wameanza kushughulikia kesi za wanachama wao waliojeruhiwa katika harakati za kuelekea mahakamani Aprili 24,2025 kusikilza kesi ya lissu.