Na Magrethy Katengu,JamhuriMedia,
Dar es Salaam
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) imelaani vikali changamoto zilizojitokeza kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikiwemo kuenguliwa wagombea, vikwazo katika ukukuaji fomu na urejeshaji,mapingamizi ya rufaa, kupotea, kutekwa na kujeruhuwa kwa baadhi ya viongozi
Tamko hilo limetoliwa Novemba 14, 2024 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania CCT Askofu Dkt Fredrick Shoo ambapo amesema jumuiya hiyo wamefuatilia kwa kina hali ya kisiasa ilivyo katika Taifa kuhusiana na mchakato mzima wa uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kuanza Novemba 27 mwaka huu na kusikitishwa sana na dosari ambazo ni madhila yaliyojitokeza 2019 yakijirudia tena wakati Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anasisitiza 4R .
” Tunaitaka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu unasimamiwa kwa haki na usawa na kuondoa changamoto zinazoathiri michakato wa uchaguzi kila wakati nchi inapoingia katika chaguzi kwani hali hii inaleta hali ya kufifisha uhuru wa kisiasa” amesema askofu Dkt Shoo.
Askofu Dkt Shoo amebainisha kuwa , kumekuwa na malalamiko juu ya uandikishaji wa daftari wawapiga kura watu wasiokuwa na sifa, kiwemo marehemu kuandikishwa, na wasiokuwa na umri halali kuandikishwa utaratibu huo wa muda mfupi wa uandikishaji wa siku saba tu hali iliyopelekeanchi watu walio nasifa kushindwa kujiandikisha.
“Kuenguliwa kwa wagombea kwa sababu ndogo za kiufundi,Vikwazo katika kuchukua na kurejesha fomu za wagombea, mapingamizi ya rufaa, kutekwa, kujeruhiwa , kupotea na kuuwa kwa wananchi kunakohusiana na masuala ya siasa na uchaguzi yote haya ni changamoto zilizobainika katika maandalizi ya Uchaguzi “amesema Askofu Dkt Shoo.
Licha ya kutoa muda wa kupeleka rufaa lakini Askofu Dkt Shoo , amevitaka vyama vya siasa kufuatilia na kusimamia kampeni za wagombea kwa ukaribu na kuhimiza ustarabu na kuelimisha katika kunadi sera za chama husika bila kutumia lugha mbaya za matusi/Maudhi zinazoweza kuhatarisha amani ya nchi.
“Tunahamasisha vyama vyote vinavyowania nafasi za uchaguzi kuweka mawakala waadilifu katika kusimamia zoezi zima la upigaji wa kura, kuhesabu, kujumlisha na kutangaza matokeo ili kuepuka sintofahamu baada ya Uchaguzi na kutupiana lawama”amesema askofu Dkt Shoo.
Aidha, amesema kuwa mgombea ambae hana mpinzani sheria inaelekeza apigiwe kura ya NDIYO na HAPANA ili kutoa haki kwa wananchi kuchagua viongozi wanaowataka na sio kupitishwa bila kupingwa, na amewashauri waumini wote kumtanguliza Mungu Mbele katika kipindi hiki muhimu wanapoelekea katika uchaguzi kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Taifa.
Sambamba na hayo ametawaka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wa mtaa, Kijiji na kitongoji wenye sifa sio kufuata ushabiki wowote ule , huku akiwataka waendelee kudumisha amani na mshikamano wakati na baada ya uchaguzi.