Chama cha Mapinduzi, kimepokea kwa mstuko mkubwa taarifa za kifo cha Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa, Bi Christina Kibiki aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiyojulikana.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Novemba 13, 2024 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla imesema kuwa marehemu alikuwa anajindaa kuhudhuria semina elekezi kwa Makatibu Mjini Dodoma kesho.
Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa familia, ndugu, viongozi na wanachama wa CCM Mkoa wa Iringa kufuatia kifo cha ghafla na cha kikatili.
“Tunawaomba wanachama wetu wawe watulivu wakati vyombo vya dola vikifuatilia na kuchunguza tukio hili, ili wahusika waweze kufikishwa katika vyombo vya kisheria” alisema.