Katibu Mkuu wa Chama Chama Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo kwa dhamana ya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa
Uchaguzi wa ndani ya chama unaoendelea huku ukifikia ngazi za mikoa chama na jumuiya, ametangaza kufuta uchaguzi
katika baadhi ya maeneo, kusimamisha mchakato wa uchaguzi na kutuma timu za uchunguzi katika maeneo mbalimbali
nchini.

Katibu Mkuu amefuta uchaguzi wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Simiyu, kwa kuwepo na tuhuma za rushwa kwa baadhi ya
wagombea na timu ya uchunguzi imeshatumwa kulifuatilia hilo kwa kina, na hatua zaidi zitachukuliwa haraka baada ya
uchunguzi kukamilika.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo


Pia, Chongolo amesimamisha uchaguzi wa nafasi ya mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Mbeya na Arusha kwa
sababu za kuwepo kwa tuhuma mbalimbali zikiwepo za rushwa, na sasa uchunguzi unaendelea na hatua zitachukulia.
Aidha, Katibu Mkuu ameeleza kuwa uchaguzi uliofanyika Novemba 20, 2022 mkoa wa kichama wa Magharibi Zanzibar,
kumekuwa na malalamiko kwa kitendo cha baadhi ya wanachama kubeba sanduku la kura na kulipeleka eneo la kuhesabia.

Zinazohusiana

CCM yawateua hawa kugombea nafasi za uongozi Taifa, Mkoa

Mwnyekiti CCM Rais Samia aongoza kikao cha Kamati Kuu CCM


hivyo timu ya uchunguzi inafuatilia na ikigundulika jambo hilo halikuwa na nia njema uchaguzi utafutwa na kuchukua hatua
zaidi.
Hata hivyo, Katibu Mkuu amewashukuru wanachama wote wa CCM kwa kuendelea na uchaguzi kwa amani na kwa utulivu
mkubwa, licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo katika baadhi ya maeneo ambapo Chama kinaendelea kufuatilia
kwa karibu na kuchukua hatua kwa haraka.