Na Isri Mohamed

KATIBU mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Dkt Emmanuel Nchimbi amezungumza na wanahabari leo kuhusiana na masuala mbalimbali ya kisiasa na kijamii yanayoendelea nchini, hususani matukio ya utekaji na mauaji yaliyotokea yakiwemo ya aliyekuwa mjumbe wa sekretarieti ya chadema, Mohamed Ali Kibao.

Katika mazungumzo yake katibu mkuu Nchimbi ameonesha kusikitishwa na kampeni iliyoanzishwa na baraza la vijana wa Chadema (Bavicha) inayoitwa ‘SAMIA MUST GO’ .

“Kuna vitu ukisema unavyojua kabisa haviwezekani, yupo pale kwa mujibu wa katiba na atamaliza muda wake kwa mujibu wa katiba, moja ya sifa za kijana anayeandaliwa vizuri anatakiwa kuanza kufundishwa kuheshimu katiba, tunaweka uchaguzi miaka mitano mitano, ili wale watakaokuwa hawaridhiki ndani yah ii miaka mitano wapate miaka mingine ya kuchagua sio katikati ya msimu uchaguzi haujafika mnaanza Fulani must go, Fulani must go”

“Wanaojua demokrasia ndio maana Mbowe ni mwenyekiti wa Chadema mpaka leo, kila zilipoanza kelele ndani ya Chadema ‘Mbowe Must Go’ zimeshindikana kwa sababu ni kinyume cha katiba yao, wanaolinda katiba ya Chadema wamemlinda Mbowe kwa nguvu zao zote, imetokea Zaidi ya mara tatu ‘Mbowe must go’ ameenda wapi? Yupo na Samia atakuwepo na Mbowe atakuwepo”

Aidha Katibu mkuu Nchimbi ameendelea kutilia mkazo agizo la Rais Samia la kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuharakisha upelelezi wa matukio hayo ili kuwabaini wahalifu wanaodhulumu haki ya watu ya kuishi.

Please follow and like us:
Pin Share