Category: Makala
Neno ‘kustaafu’ nalo ni tatizo!
Joe Beda Rupia Kustaafu ni kama kifo. Ndiyo. Ukianza kazi siku ya kwanza tu, unaanza safari ya kustaafu. Hakika utastaafu na neno hili linaweza kuwa chanzo cha tatizo. Sawa. Kwa wiki mbili zilizopita nimekuwa nikiandika tanzia; kwanza ya Jenerali Tumainiel…
Mke kutoa matunzo kwa mume likoje kisheria?
Na Bashir Yakub Kisheria ndoa inapokuwa imefungwa kuna haki za msingi ambazo huibuka. Hizi huitwa haki za moja kwa moja (automatic right). Huitwa haki za moja kwa moja kwakuwa hazina uhiari katika kutekelezwa kwake. Kuwapo kwa ndoa ndiko kuwapo kwake, hivyo haihitaji mtu kuziomba. Kimsingi haki hizi zipo nyingi, ambapo tutaona baadhi yake hapa, huku makala ikijikita katika haki moja ya matunzo kwa wanandoa. 1. Baadhi ya haki zinazoibuliwa na ndoa (a) Haki ya tendo la ndoa. Hii ni haki ya lazima kwa wanandoa na kutokuwapo kwake kunaweza kubatilisha ndoa iwapo mmoja wa wanandoa ataamua kufanya hivyo. Ni haki ambayo huchukuliwa kama ndiyo ndoa yenyewe, hivyo kuifanya kuwa na umuhimu wa pekee. ( b ) Haki ya kutumia jina la mume. Hii ni haki aliyonayo mwanamke ambapo anaruhusiwa kutumia jina…
Kodi ya simu za mkononi haiepukiki
Na Deodatus Balile Alhamisi, Aprili 10, 2021 Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, aliwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022. Kwanza kabla sijaijadili bajeti hii, naomba nimshukuru Mheshimiwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, kwa kulialika Jukwaa la Wahariri…
Uwekezaji: Fursa ya kuichangamkia – (2)
DAR ES SALAAM Na Mwandishi Wetu Wiki iliyopita tulitazama namna ambavyo kampuni ya uwekezaji wa pamoja inayomilikiwa na serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango inavyofanya tathmini na utafiti wa kina kabla ya kuwekeza fedha zilizokusanywa. Endelea… Tofauti ni nyingi,…
Binti Arusha aweka rekodi
ARUSHA Na Hyasinti Mchau Binti wa Arusha, Rawan Dakik (20), ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza mwanamke kupanda Mlima Everest. Mlima huo uliopo nchini Nepal, barani Asia, ndio mrefu kuliko yote duniani, kilele chake kikiwa mita 8,849. Rawan, amerejea…
Nafasi ya mwanamke katika Uislamu
Makala hii yenye anuani ‘Nafasi ya mwanamke katika Uislamu’ inakusudia kuweka wazi namna Uislamu ulivyompa heshima mwanamke, kinyume cha yale madai kuwa Uislamu umemdhulumu mwanamke na umemnyima haki zake mbalimbali. Wakati mwingine madai kama haya yanatokana na kukosa kipimo sahihi…