Category: Makala
Hongera MCT, lakini namna ya kuwapata washindi itazamwe
Baraza la Habari Tanzania (MCT) limetoa tuzo kwa waandishi wa habari, wachora katuni na wapigapicha bora. Hili ni tukio jema. Linapaswa kuungwa mkono. Rais Jakaya Kikwete ameliona hilo, ameahidi kuwa Serikali itashiriki.