Category: Makala
Hotuba iliyowazima wabunge mafisad
Bunge linanuka rushwa. Baadhi ya wabunge wanapokea rushwa ili kutetea maslahi ya wanaowatuma. Lakini wapo wabunge jasiri walioamua kupambana na wenzao wala rushwa kama inavyothibitishwa na Hotuba ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Wizara ya Nishati na Madini,…
Biashara za sasa zinahitaji u-sasa
Wakati baba yangu mzazi akifariki katikati ya miaka ya 1990, alikuwa mmoja wa wafanyabiashara waliokuwa wakipanda kwa kasi kubwa kibiashara. Akiwa ameshakusanya uzoefu wa kusafiri kibiashara hadi nchi jirani ikiwamo Malawi, alifariki dunia na kuacha biashara zilizokuwa zimestawi kweli kweli.
Ewura yaokoa bilioni 170/-
*Ni baada ya kudhibiti uchakachuaji kwa kuweka vinasaba
*Wabunge waliotemeshwa ulaji wanaanza harakati ivunjwe
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeliwezesha taifa kuokoa zaidi ya Sh bilioni 170 kwa mwaka, lakini hatua hiyo imewakera baadhi ya wabunge waliokuwa wakichakachua na sasa wanafanya mbinu ivunjwe.
Hotuba ya Upinzani iliyozuiwa bungeni hii hapa
Wiki iliyopita Serikali iliibua hoja na kufanikiwa kuzuia baadhi ya maneno yaliyokuwamo kwenye hotuba ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzanji Bungeni wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Vincent Nyerere, yasisomwe. JAMHURI inakuletea hicho kilichozuiwa kusomwa.
Siri ya mafanikio yangu kiuchumi – 2
Wiki iliyopita nilieleza namna changamoto za kiuchumi zinavyowahenyesha wafanyakazi. Pia nilianza kueleza mchapo unaonihusu wa namna nilivyopambana kujikwamua kiuchumi nikiwa nimeajiriwa kwa kazi ya ualimu. Leo nitahitimisha kwa kubainisha mbinu kadhaa ili kumudu mchakamchaka wa maisha ya kiuchumi. Endelea…
Museveni: Waafrika hatujui kuomba
“Tatizo letu sisi Waafrika hatujui kuomba, na hata tunapopata fursa ya kuomba hatuombi kwa akili. Nilipokwenda kwa Gaddafi [wakati napigana vita ya kumuondoa Idi Amin) aliniuliza ‘Nikupe pesa?’ Nikasema hapana. Akasema ‘Nikupe sare za askari?’ Nikamwambia hapana. Akasema ‘Unataka nini sasa kwangu?’ Nikamwambia bunduki na risasi.”