Category: Makala
Mgogoro wa Tanzania, Malawi ngoma mbichi
*Malawi waendelea kukomaa wachukue ziwa lote
*Tanzania yasema mgawo ni nusu kwa nusu tu
*Wazee wa hekima Afrika kuitwa kusuluhisha
*Wasipoafikiana kutinga Mahakama ya ICJ
*Yote hayo yakishindikana JWTZ wataamua
Kumekuwapo desturi ya wanasiasa kutafuta jambo la kuwawezesha kuwajenga kisiasa, ili waweze kushinda uchaguzi, hasa Uchaguzi Mkuu. Mzozo wa mpaka wa Ziwa Nyasa unaozihusisha nchi za Tanzania na Malawi unatajwa kuwamo mwenye mtiririko huo wa kidesturi. Malawi inatarajia kuingia kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2014, hivyo kete inayotumiwa na chama cha Rais Joyce Banda, pamoja na vyama vingine vya siasa ni kutaka kutunisha msuli kupitia mzozo wa mpaka kati yao na Tanzania kwa lengo la kujipa kuungwa mkono na Wamalawi wengi.
Bunge la sasa linaelekea wapi? (3)
Kwa namna mwenendo unavyoonekana katika Bunge, nashauri waheshimiwa wabunge wauzibe ule ufa namba tatu, ulioelezwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, unaotikisa Taifa letu. Ufa huo ni ule wa “Kuendesha mambo bila kujali sheria (Nyufa: uk. 14 ibara ya pili)”
Tujifunze kutokuwa wavivu wa kufikiri
Kati ya viongozi waliowahi kuiongoza nchi yetu na nitakaoendelea kuwaheshimu sana na kuwapenda ni Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.
Wamiliki wa daladala na machozi yasiyokauka
Baada ya kununua basi dogo (Hiace) la kwanza na kulisajili daladala, nilikutana na ulimwengu mpya wa changamoto za biashara za magari. Changamoto zilipozidi niliazimu kukutana na walionitangulia kwenye biashara hiyo ili nipate hazina ya ushauri.
Baraza la Kata Kwashemshi tupewe semina
Mimi ni msomaji wa Gazeti Jamhuri. Naishi hapa Kwashemshi wilayani Korogwe. Kinachosikitisha ni kwamba tangu mwaka jana tuteuliwe katika Baraza la Kata hakuna semina yoyote ambayo wajumbe tumepewa. Sasa inatuwia vigumu kwetu kutafsiri sheria. Hali hii ni kinyume kabisa…
Bongo: Matendo kwanza
“Ni wajibu wa viongozi wa Afrika kuonyesha utashi wao wa kisiasa, kwa ajili ya kuhakikisha taasisi za umajumui wa Kiafrika (pan-African) unakuwa chombo murua na kisiwe chombo cha mijadala isiyo na ukomo.”
Haya ni maneno ya aliyekuwa Rais wa Gabon, Omar Bongo, aliyefariki mwaka 2009 baada ya kuitawala nchi hiyo kwa muda mrefu.