Category: Makala
Nani anawashika mkono wajasiriamali?
Mwezi mmoja uliopita niliandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari “Barua ya biashara kwa BRELA”. Brela ni Mamlaka ya Uandikishaji Biashara na Leseni. Baada ya kuitoa gazetini niliituma pia barua hiyo huko Brela kwa njia ya barua pepe.
TAFAKURI YA HEKIMA
Polisi wangeweza kuepusha mauaji ya Mwangosi
Nianze kwa kutoa salamu za rambirambi na pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na watu wote walioguswa na kifo cha mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, amina.
Wafadhili wa migogoro Loliondo wajulikana
Suala la mgogoro wa Loliondo limekuwa likitawala katika vyombo vya habari kwa miongo kadhaa sasa. Safari hii kuna kampeni inayoendeshwa kwenye mtandao kwa wiki kadhaa sasa. Chanzo cha mjadala huo ni kwamba Serikali ya Tanzania inataka kuwaondoa wafugaji wa Kimasai ndani ya Loliondo ili kupisha biashara ya uwindaji wa kitalii. Kampeni hiyo inaendeshwa na mtandao wa Avaaz.
China yaipatia Zanzibar mabilioni
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China zimetiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kiufundi ambako Zanzibar itapatiwa Sh bilioni 14.8.
Kikwete polisi wanaanza kuyeyusha heshima uliyojijengea
Mwaka 2008 nilibahatika kuwa mmoja wa watu waliopata fursa ya kusafiri na Rais Jakaya Kikwete kwenda jijini Washington, Marekani. Safari hii ilikuwa ikihusiana na mambo mbalimbali lakini kubwa ni kushawishi Serikali ya Marekani kuridhia Mpango wa Millennia Challenge Cooperation (Account) – MCC.
Waziri Mgimwa ahimiza ufanisi PPF
Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, amehimiza utendani makini utakaongeza ufanisi katika Mfuko wa Pensheni za Mashirika ya Umma (PPF) nchini.