Category: Makala
Natamani serikali ya China ingekuwa Tanzania
Waswahili siku zote husema adaa ya mja kunena, muungwana ni kitendo. Serikali ya China ni mfano mzuri wa kuigwa kwa jinsi inavyosimamia sheria, sera na taratibu zake kwa vitendo. Natamani serikali ya China ingekuwa Tanzania ili, pamoja na mambo mengine, ishughulikie kwa vitendo watumishi wanaotumia vibaya madaraka na ofisi za umma.
Utaifa hauna dini (1)
Wakoloni, hasa Waingereza, walikuwa na ubaguzi wa hali ya juu. Miongoni mwa raia wao walikuwapo walioitwa raia halisi (British nationals), na raia watawaliwa (British subjects).
Dk. Hoseah aomba majina ya walioficha mabilioni Uswisi
*Asema Takukuru haizuii watu kujenga mahekalu
*Wadau wataka wanaothibitika kula rushwa wauawe
Ujasiri na ushirikiano wa dhati vimetajwa kuwa ni miongoni mwa nyenzo thabiti, zinazoweza kuongeza ufanisi katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa nchini.
Afadhali ya ‘ngangari’ kuliko ‘magwanda’ haya (1)
Si siri kuwa tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini, mambo si shwari. Amani na utulivu wa nchi yetu vimetikisika. Nadiriki kusema hivi kwa sababu, tangu Uchaguzi Mkuu wa kwanza uliofanyika mwaka 1995, amani na utulivu vimekuwa vikiyumba kila kukicha.
Wingi wa sukari maghalani wamkera Waziri Chiza
*Ahoji sababu ya kutouzwa, akerwa na bei ghali ya sukari
*Akataa kuruhusu iuzwe nje, Mkurugenzi wa Bodi amkwaza
Wakati Watanzania wakiumizwa na bei ghali ya sukari, imebainika kuwa karibu tani 180,000 za bidhaa hiyo ‘zinaozea’ maghalani katika Jiji la Dar es Salaam na sasa wafanyabiashara wanasaka kibali cha kuiuza nje ya nchi.
Baada ya Ziwa Nyasa, mgogoro sasa waibuka Ziwa Kitangiri
Umiliki wa Ziwa Kitangiri unafanana na mgogoro uliopo sasa wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi katika Ziwa Nyasa. Wakati mgogoro wa Malawi ukipewa kipaumbele, huu wa Ziwa Kitangiri linalotenganisha wilaya za Meatu na Iramba haujapewa msukumo wa kutosha.