JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Makala

Yah: Nimeoteshwa ndoto ni nani rais ajaye?

Wanangu, leo najua ni Jumanne nyingine ambayo mtakuwa mnatafakari mustakabali wa maisha yenu baada ya kuwa kila siku inayopita mnaona nafuu ya jana. Haya yote yawezekana ni kutokana na kosa lenu la kupiga kura katika kumchagua kiongozi wako kuanzia ngazi ya tawi hadi juu kabisa.

 

Butoto atamani maendeleo Kabilizi

“Nina karibia kustaafu na kutoka mjini nirudi kijijini nikaungane kimawazo na kivitendo na wananchi wenzangu kuikomboa Kata ya Kabilizi katika Jimbo la Muleba Kusini.’’

Mwalimu Nyerere: Kujitolea kumefifia

“Siku hizi kuna watu wengi mno ambao huingia katika chama na kugombea nafasi za uongozi kwa matumaini ya kupata fedha na vyeo kwa faida zao wenyewe. Moyo wa kujitolea umefifia mno. Katika hali kama hiyo ni vigumu sana kuwapata viongozi wenye moyo wa kuwatumikia wenzao.”

Haya ni maneno ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Nyerere, wakati akikemea tabia ya wanaotafuta uongozi kwa ajili ya maslahi yao binafsi. Alizaliwa Aprili 13, 1922 kijijini Butiama, Mara, alifariki Oktoba 14, 1999 jijini London, Uingereza.

Julius Nyerere: Tukiendeleze Kiswahili

“Pamoja na kwamba mimi binafsi napenda tuendelee kufundisha Kiingereza katika shule zetu, kwa sababu Kiingereza ndicho Kiswahili cha Dunia, tuna wajibu mkubwa kuzidi kukiendeleza na kukiimarisha Kiswahili: Ni silaha kubwa ya umoja wa Taifa letu.”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, yanayopatikana katika moja ya hotuba zake kwa umma. Alizaliwa Aprili 13, 1922 kijijini Butiama, Mara na kufariki Oktoba 14, 1999 jijini London, Uingereza.

Kuna umuhimu wa wafanyabiashara ‘kuolewa Bongo’

Novemba 11, mwaka huu, nilikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria semina ya biashara na ujasiriamali katika ukumbi wa Matumaini Centre, uliopo Sabasaba Iringa mjini. Semina hii iliendeshwa na mtaalamu na mshauri wa kimataifa wa masuala ya biashara na ujasiriamali, Perecy Ugula, kupitia kampuni yake ya Great Opportunity Consulting Limited (GOC Ltd).

Serikali isipuuze, udini upo, iudhibiti

Naanza maelezo yangu kwa kusema yafuatayo: Msema kweli hukimbiwa na marafiki zake; siwezi kuikana kweli kwa kuchelea upweke wa kitambo; nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.