Category: Makala
Tuwakubali Ili wakubalike
Vipaji vipo kila kona ya dunia, lakini ili kipaji kikue ni lazima kwanza kikubalike nyumbani kabla hakijakubaliwa ugenini. Kipaji hakipatikani shuleni, kipaji unazaliwa nacho na unakua na kutembea nacho, na ili kipaji kionekane na watu wengine unatakiwa ukioneshe.
Bunge lisifanyie mzaha matumizi ya fedha za rada
Nianze kwa kuwaomba kila mbunge anayetambua kuwa amechaguliwa na wanyonge na maskini wa Tanzania ili atetee maslahi yao na ya watoto wao, asome kwa makini makala haya kisha achukue hatua.
Je, Mkristo akichinja ni haramu?-5
Wiki iliyopita tulikuletea sehemu ya nne ya makala haya yanayohoji usahihi juu ya nani anastahili kuchinja. Leo tunakuletea sehemu ya tano na ya mwisho ya makala haya. Endelea….
Ndivyo itakavyokuwa hata kwenye kitoweo kingine na serikali itakusanya kodi zake kwa uwazi zaidi kuliko ilivyo sasa ambapo huenda wengine wanachinjia nyumbani kwao kwa siri halafu wanapeleka maeneo ya biashara na kuikosesha kodi serikali.
Sisi Waafrika weusi tukoje? (4)
Nchini mwetu, licha ya kilio cha Baba wa Taifa kuacha ufahari na matumizi ya magari makubwa, lakini ukienda Mbezi Beach, au Jangwani Beach, au hata hapo Oysterbay, mtu unashangazwa na mijumba mikubwa ya watumishi wa umma yanavyoumuka kama uyoga vile.
NUKUU ZA WIKI
Nyerere: Moyo wa kujitolea umefifia
“Moyo wa kujitolea umefifia mno. Katika hali kama hiyo ni vigumu sana kuwapata viongozi wenye moyo wa kuwatumikia wenzao.”
Mameno haya ni ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Utalii uzalishe ajira kwa wananchi
Sekta ya utalii inatajwa kuwa ya pili katika kuchangia pato la Taifa kutokana na fedha za kigeni, lakini pia ina fursa nyingi zinazoweza kuzalisha ajira kwa watu wanaozunguka maeneo husika.