Category: Makala
BARUA ZA WASOMAJi
Barua ya wazi kwa Waziri wa Maji
Mheshimiwa Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, hongera kwa kazi, siwezi kukupa pole kwani kazi ni wajibu na kipimo cha mtu.
Ansar Sunni: Hatumtambui Sheikh Ponda
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu wa Ansar Sunni, Sheikh Salim Abdulrahim Barahiyan, amesema jumuiya hiyo haina uhusiano na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Waislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda. “Mimi sijawahi kukaa na Sheikh Ponda katika kikao hata kimoja. Tuna misikiti karibu 20 Tanga, hajawahi kuingia hata msikiti mmoja,” amesema Sheikh Barahiyan.
Barua ya wazi kwa Waziri Mwakyembe
Mheshimiwa Waziri Dk. Harrison Mwakyembe, tunayo heshima kuchukua nafasi hii kukujulisha kuwa matrekta haya unayoyaona yamekwishalima sana na sasa hayawezi kazi hiyo tena. Ukiyafukuza mjini ni wazi hayatakwenda kulima, maana mengi hayana uwezo tena wa kufanya kazi hiyo.
MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE
Tujisahihishe: Mwalimu Nyerere
UMOJA wa kundi lolote ni sawa sawa na umoja wa viungo mbalimbali vya mwili au mtambo. Viungo vya mwili havina budi vitii kanuni zinazoviwezesha kufanya kazi yake sawa sawa. Lakini haviwezi kutii kanuni hizo kama haviko katika hali ya afya njema. Mara kiungo kimoja kinapokuwa hakina afya safi, huanza kuvunja kanuni za kazi na mwili mzima hupata taabu.
KAULI ZA WASOMAJI
Wanahabari tembeleeni pia vijijini
Waandishi wa habari jaribuni kutembelea pia na maeneo ya vijijini kwa sababu huko kuna matukio mengi ya kutisha na kusikitisha, lakini vyombo vya habari vimekuwa havielekezi nguvu kubwa vijijini kama vinavyofanya maeneo ya mijini.
Obe Mlemi, Mugumu – Serengeti
0768 235 817
Ukitaka mafanikio halisi lipa kodi kwa uaminifu
Kwa hivi sasa mashine za kielektroniki za EFD za TRA, imekuwa ndiyo habari ya ‘mjini’ kwa wafanyabiashara karibu kila kona nchini. Hii imekuja baada ya awamu nyingine ya TRA kujumuisha wafanyabiashara wengi zaidi tofauti na ilivyokuwa mwanzo wakati zikiingia.