Category: Makala
JAMHURI YA WAUNGWANA
Kuanzia kitongoji hadi
Ikulu wote wanalalamika
Siku kadhaa zilizopita nilikutana na mwanahabari mwenzangu, Khalfan Said. Aliniuliza swali hili; “Huu uamuzi wa Rwanda na Uganda kususa bandari zetu utakuwa na athari gani kwa uchumi wetu.” Khalfan aliniuliza swali hili akitambua kuwa mimi si mchumi. Hilo analitambua vema. Mara moja nikatambua kuwa tunao kina Khalfan wengi wanaotaabishwa na jambo hili, kiasi kwamba wapo radhi kumuuliza yeyote wanayemwona hata kama wanajua si mtaalamu wa masuala ya uchumi.
Meya, mbunge Ilemela bado kunachimbika
Mgogoro baina ya Meya wa Manispaa ya Ilemela, Mstahiki Henry Matata, na Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia, unaendelea kufukuta na kujenga makundi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Hatujajipanga kuleta BRN katika elimu
Baada ya kuona kuwa wameboronga elimu na wameendelea kusemwa vibaya, sasa Waziri wa Elimu na wasaidizi wake wamekuja na jambo jipya kwa lengo la kujikosha. Wamekuja na mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now-BRN).
Utata wagubika mradi wa umwagiliaji Nyamboge-Nzera
Ndoto ya wakazi wa vijiji vya Nyamboge na Nzera katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ya kuendesha kilimo cha umwagiliaji imepotea.
FIKRA YA HEKIMA
LAAC imechelewa kugundua
madudu hazina, halmashauri
Ijumaa iliyopita, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ilitangaza kugundua mtandao wa wizi wa mabilioni ya shilingi za umma. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Rajab Mohamed Mbarouk, alisema mtandao huo unahusisha ofisi za Hazina na halmashauri mbalimbali hapa nchini.
TBS yadhibiti uharibifu injini za magari
Kuzinduliwa kwa mtambo mpya wa kupima mafuta kunaashiria kwisha kwa tatizo la muda mrefu la kuharibika kwa injini za magari yanayotumia mafuta ya petroli nchini. Mtambo huo wa kisasa uliozindulia wiki iliyopita na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda, jijini Dar es Salaam, ni miongoni mwa mitambo inayopima mafuta ya magari iliyopo katika maabara ya kemia.