JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Makala

NUKUU ZA WIKI

Julius Nyerere: Kumteta mtu ni kumdhuru

“Wengine humwona mwenzao anafanya kosa, badala ya kumwambia pale pale kijamaa kwamba atendalo ni kosa, watanyamaza kimya. Lakini hawanyamazi kabisa! Watakwenda kumteta katika vikundi vya siri siri. Mateto haya si ya kumsaidia mwenzao, ni ya kumdhuru.”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Ndiye Rais wa Kwanza wa Tanganyika na baadaye Tanzania.

Tumetoka wapi, tupo wapi, tunakwenda wapi

Hotuba ya Mwalimu Julius K. Nyerere Aliyoitoa Wakati wa Kilele cha

Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani, Mbeya, Mei Mosi, 1995.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alialikwa kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika kitaifa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya,  Mei Mosi, 1995. Katika hotuba yake, Mwalimu alielezea historia ya vyama vya wafanyakazi duniani. Aidha, alitumia fursa hiyo kutoa maoni yake kuhusu hali ya kisiasa na kiuchumi nchini pamoja na ushauri kuhusu mambo wananchi wanayopaswa kuzingatia wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huo, hasa sifa za wagombea nafasi za uongozi kuwa ni pamoja na kila mmoja kujiuliza ataifanyia nini nchi yake baada ya kuchaguliwa, na anakwenda kufanya nini Ikulu. Ifuatayo ni hotuba ya Mwalimu…

Navumilia kuwa Mtanzania

Tanzania ni nchi yangu ninayoipenda kwa moyo wote, ni kisiwa cha amani, upendo na utulivu, ni nchi yenye watu wakarimu na wenye upendo na mahaba yasiyopimika. Watanzania wanaishi kwa kupendana kuthaminiana na kuheshimiana bila kujali matatizo au changamoto zinazowakabili, kila mmoja akimuita mwenzake ndugu.

JAMHURI YA WAUNGWANA

Kuanzia kitongoji hadi
Ikulu wote wanalalamika

Siku kadhaa zilizopita nilikutana na mwanahabari mwenzangu, Khalfan Said. Aliniuliza swali hili; “Huu uamuzi wa Rwanda na Uganda kususa bandari zetu utakuwa na athari gani kwa uchumi wetu.” Khalfan aliniuliza swali hili akitambua kuwa mimi si mchumi. Hilo analitambua vema. Mara moja nikatambua kuwa tunao kina Khalfan wengi wanaotaabishwa na jambo hili, kiasi kwamba wapo radhi kumuuliza yeyote wanayemwona hata kama wanajua si mtaalamu wa masuala ya uchumi.

Meya, mbunge Ilemela bado kunachimbika

Mgogoro baina ya Meya wa Manispaa ya Ilemela, Mstahiki Henry Matata, na Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia, unaendelea kufukuta na kujenga makundi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Hatujajipanga kuleta BRN katika elimu

Baada ya kuona kuwa wameboronga elimu na wameendelea kusemwa vibaya, sasa Waziri wa Elimu na wasaidizi wake wamekuja na  jambo jipya kwa lengo la kujikosha. Wamekuja na mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now-BRN).