Category: Makala
Mwigulu kata pua uunge wajihi
Juma lililopita nikiwa nafuatilia Kikao cha Pili cha Mkutano wa Bunge, nilimshuhudia na kumsikia Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, akieleza matukio ya vifo vya raia katika maeneo kadhaa nchini, vilivyotokea kwenye shughuli za kisiasa na akahoji nafasi ya kisheria kuwashughulikia wahusika na waratibu wa matukio hayo badala ya wale wanaoshiriki katika maelezo yake.
Matakwa ya Rwanda yasiivunje EAC
Kwa muda wa mwezi mmoja sasa uhusiano baina ya Tanzania na Rwanda umezorota. Uhusiano huo umezorota baada ya matukio mawili. Tukio la kwanza ni ushauri Rais Jakaya Kikwete aliompa Rais Paul Kagame wa kuzungumza na waasi wa kundi la FDLR kwa nia ya kurejesha amani. La pili ni Tanzania kupeleka majeshi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kupambana na waasi wa M23.
Hii ndiyo dawa ya kuepuka bomoabomoa
Katika miaka ya 1980, bendi moja ya muziki wa dansi hapa nchini ilitunga wimbo uliokuwa na kibwagizo cha “bomoa ee, bomoa ee, tutajenga kesho!”
Misitu inavyoinufaisha Nanjilinji ‘A’ (5)
Katika sehemu ya nne, Dk. Felician Kilahama alizungumzia kazi ya kutoa huduma bora za kijamii na kujenga miundombinu imara katika nchi yenye eneo kubwa. Alisema shughuli hiyo inahitaji ujasiri mkubwa na uzalendo wa hali ya juu. Sehemu hii ya tano na ya mwisho, Dk. Kilahama anatoa hitimisho.
MISITU & MAZINGIRA
Misitu inavyoinufaisha Nanjilinji ‘A’ (4)
Pongezi kwa wananchi wa Nanjilinji ‘A’
Kwa kuzingatia mafanikio yaliyopatikana katika Kijiji cha Nanjilinji ‘A’ na kwa kuelewa kuwa mafanikio hayo yametokana na wanakijiji kudhamiria kwa dhati kutumia rasilimali misitu inayopatikana ndani ya mipaka ya kijiji chao bila kushurutishwa na mtu yeyote, napenda nichukue fursa hii kutoa pongezi zangu za dhati kwa uongozi wa kijiji na wakazi wake wote kwa mafanikio hayo ya kutia moyo.
KONA YA AFYA
Vidonda vya tumbo na hatari zake (10)
Wiki iliyopita, Dk. Khamis Zephania alielezea dalili za vidonda vya tumbo yakiwamo maumivu na tofauti yake kulingana na rika. Sasa endelea kumfuatilia katika sehemu hii ya kumi…