JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Makala

Hotuba iliyochafua hali ya hewa ndani ya Bunge

MAONI YA MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA SHERIA NA KATIBA, MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU KUHUSU
MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA, YA MWAKA 2013

(Kanuni ya 86(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2013)

 

UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika,

Huu ni Muswada wa marekebisho ya pili ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya Sheria za Tanzania. Kama Bunge lako tukufu litakavyokumbuka, Sheria hii ilifanyiwa marekebisho ya kwanza kwa kupitishwa kwa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Na. 2 ya mwaka 2012, mwezi Februari ya mwaka jana. Mabadiliko hayo ya kwanza yalihusu Sehemu ya Tatu na ya Nne ya Sheria hii, na yalilenga vifungu mbali mbali vinavyohusu Tume ya Mabadiliko ya Katiba na utekelezaji wa majukumu yake.

Tanzania na biashara za kishirikina

Wiki iliyopita niliandika makala yaliyokuwa na kichwa, “Je kufanya biashara ni kipaji?” Ninafurahi kuwa yamekuwa makala yaliyowavutia wengi ambao hawakusita kunitumia mirejesho ya pongezi na maoni kupitia ujumbe wa simu, barua pepe na simu za miito. Msomaji mmoja amenitumia ujumbe ulionifurahisha kweli kweli; ninanukuu, “Makala yako ni nzuri na umechambua kitaalamu, lakini pia utajiri wa Wakinga asilimia 70 huwezi kuutenganisha na ushirikina. Vile vile Wachagga nao utajiri wao asilimia 30 ni ushirikina na 20% ni ujambazi. Na asilimia zilizobaki ndizo zinazoangukia kwenye uchambuzi wako,”  mwisho wa kunukuu. Leo nitachambua kwa mara nyingine tena hili sekeseke la ushirikina kuhusishwa na biashara, si tu kwa Wakinga na Wachagga pekee, bali pia kwa wafanyabiashara wote bila kujali kabila wala eneo waliloko. Lakini kabla ya kuendelea na uchambuzi huu kwanza nina taarifa moja ya muhimu kwa wasomaji wetu.

NUKUU ZA WIKI

Julius Nyerere: Nchi haiendelei bila viwanda vya kisasa

“Maana ya maendeleo ya leo ya uchumi wenye nguvu ni maendeleo ya viwanda. Nchi yenye viwanda tunasema ni nchi iliyoendelea. Hata hivyo, tuna maana nyingine ya nchi zilizoendelea ya kuziita ni nchi zenye viwanda. Nchi haiwezi kuendelea bila kuwa na viwanda vya kisasa.

FIKRA YA HEKIMA

Kampuni za simu za mkononi  zinaiba umeme, hatutapona

Wakati Wizara ya Nishati na Madini ikiwaaga vijana 10 wazawa wanaokwenda China kusomea shahada ya uzamili kuhusu fani ya mafuta na gesi wiki iliyopita, Shirika la Taifa la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kubaini wizi wa nishati ya umeme kwenye minara ya kampuni za simu za kiganjani.

KONA YA AFYA

Vidonda vya tumbo na hatari zake (11)

Katika sehemu ya kumi, Dk. Khamis Zephania alifafanua maumivu ya vidonda vya tumbo, tofauti ya vidonda hivyo na vile vya duodeni, sababu za kutosagika kwa chakula na mtu kupungua uzito. Sasa endelea…

BARUA ZA WASOMAJi

Polisi Biharamulo wanatumaliza

Kwa kawaida tunajua kuwa mtu akiwa mikononi mwa askari polisi atakuwa yuko kwenye usalama, lakini huku wilayani Biharamulo, Kagera hilo halipo.