Category: Makala
Nyerere alitabiri madhara ya uuzaji ardhi
Oktoba 14, mwaka huu Watanzania tuliadhimisha miaka 14 ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Ifuatayo ni makala iliyoandaliwa na MWANDISHI WETU kwa msaada wa blogu ya Udadisi, ikielezea mtazamo wa kiongozi huyo kuhusu uzaji ardhi.
“Katika nchi kama yetu, ambamo Waafrika ni masikini na wageni ni matajari, kuna uwezekano mkubwa kwamba Mwafrika akiruhusiwa kuiuza ardhi yake katika miaka themanini au mia moja ijayo, ardhi yote ya Tanganyika itamilikiwa na matajiri wageni na wenyeji watakuwa watwana. Lakini hata kama wageni wasingekuwa matajiri, litaibuka tabaka la Watanganyika matajiri na wajanja. Tukiruhusu ardhi iuzwe kama kanzu, katika muda mchache kutakuwa na kundi dogo la Waafrika wakiwa na ardhi na walio wengi watakuwa watwana.” JKN 1958 (Uhuru na Umoja)
KIFO CHA NYERERE NI UTATA
Tangu mwaka jana juhudi za chini chini zilianza kufanywa na baadhi ya Watanzania ambao hawajaridhika kuwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alifariki kifo cha kawaida.
Nakulilia Nyerere, wanakulamba kisogo
Ni miaka 14 sasa tangu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alipoaga dunia Oktoba 14, 1999 katika HospitalI ya St. Thomas jijini London. Ilikuwa siku ya majonzi makubwa kwa Watanzania kumpoteza mtu aliyetumainiwa na wengi kama nguzo na dira ya maono kwa Taifa la Tanzania.
Yah: Maskini Nyerere alikufa hana nyumba!
Nimeamua kuandika waraka huu maalum kwenu kizazi cha dotcom, kwa lengo la kutaka kuwakumbusha sisi tulifanya nini katika kuhakikisha nchi hii inafika tulikokuwa tunataka kabla ya ninyi kuamua kulivunja Azimio la Arusha.
Miigo: Nyerere alitumia ‘media’ kuhamasisha ukombozi Afrika
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ametajwa kuwa kiongozi aliyependa kutumia vyombo vya habari kuhamasisha ukombozi wa nchi za barani Afrika kutoka katika utawala wa kimabavu wa Wakoloni.
‘Kikipatikana chama kama CCM ya Nyerere kitatawala milele’
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alidhamiria kuifanya Tanzania kuwa paradiso.