Category: Makala
FASIHI FASAHA
Vyama vya upinzani ni vichanga? -2
sehemu ya kwanza ya makala haya, wiki iliyopita nilizungumzia chimbuko la vyama vingi vya siasa kabla na baada ya Tanzania kuwa huru. Leo tunaendelea na sehemu ya pili.
Baada ya vyama vya TANU na ASP kuwa imara katika harakati za kudai uhuru, vyama vingine vingi vilianzishwa vikiwa na malengo ama vya kudai uhuru au kupinga harakati za kupigania uhuru na kuendeleza maslahi ya wakoloni kwa mfano, Kule Zanzibar vyama kama Zanzibar and Pemba People Party ZPPP, Umma Party vilianzishwa.
Mambo muhimu kuanzisha biashara
Biashara ni pamoja na hali ya kununua na kuuza kuzalisha mali na kuuza utaalamu wito na makubaliano ya kipekee yenye lengo la kibiashara kwa nia ya kupata faida.
Vuta nikuvute Kituo cha Mabasi Ubungo
Wadau mbalimbali wanaotoa huduma za aina tofauti katika Kituo cha Mbasi yaendayo mikoani na nje ya ncha cha Ubungo jijini Dar es Salaam wamehushutuma uongozi wa kituo hicho kwa kile walichokiita kuwa ni utaratibu mbovu wa uendeshaji.
MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE
Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (4)
Huu ni mtiririko wa maandishi yaliyomo kwenye kitabu cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania kilichoandikwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwaka 1994. Sehemu iliyopita, Mwalimu alisema, “Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili – ya Zanzibar na ya Tanganyika – kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar. Wapendao Utanganyika watakuwa wazalendo zaidi, badala ya kuwa wasaliti, wakiazimia Afrika ya Mashariki iliyoungana kuwa Nchi Moja, kuliko Tanzania iliyotengana ikawa nchi mbili.” Endelea…..
Siku ya pili yake tarehe 15:8:1993, Wabunge wenye hoja yao, na wengine zaidi, waliomba tena kuja Msasani ‘Tunywe chai’. Na baada ya mazungumzo nao ilikuwa ni dhahiri kabisa kwangu, kwamba hata kama hawakuondoa hoja yao, (wala mimi sikuwaomba waiondoe), wataitumia kutoa dukuduku zao tu; hawataitumia kung’ang’ania kudai Serikali ya Tanganyika.
JK onesha urais na usiwe mrahisi
Napenda kuchukua fursa hii kumpa pole Rais Jakaya Kikwete kwa majukumu mazito yanayomkabili kwenye uendeshaji wa Serikali, kutokana na mikinzano na vitisho anavyopata kutoka kwa baadhi ya wabunge na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
BARUA ZA WASOMAJi
Pongezi za dhati kwa Mzee Halimoja
Ndugu Mhariri,
Sina budi kutoa pongezi za dhati kwa Mzee Yusufu Halimoja kwa kazi nzuri sana ya kuendelea kutetea bila kuchoka uboreshaji wa elimu nchini.