Category: Makala
Mteja na Sayansi ya kununua
Nianze kwa kuwasalimu wasomaji wa gazeti hili, pamoja na wapenzi wa safu hii. Kwa takribani wiki nne sikuwapo hewani kutokana na sababu kadhaa ikiwamo kutingwa na shughuli za kiujasiriamali.
Gesi yabadili utamaduni Mtwara
Wiki hii Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (pichani), amefanya ziara ya siku tatu mkoani Mtwara kuangalia maendeleo ya ujenzi wa bomba la gesi. Nimepata fursa ya kuwamo kwenye ziara hii. Nimeshuhudia mengi.
MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE
Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (6)
Wiki iliyopita tulikuletea sehemu ya tano ya mtiririko wa maandiko ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere juu ya Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania. Katika kitabu alichokiandika mwaka 1994, Mwalimu alisema: “Ati Chama hakiwezi kupinga Bunge lake, lakini kwa mantiki ya ajabu ajabu wabunge wanaweza kupinga chama chao! Hiyo ndiyo demokrasia halisi ya mageuzi. Nilirudi Butiama nikalipa ada yangu ya CCM na nikaandika utenzi wa Tanzania Tanzania!” Endelea…
Jukumu la kueleza taarifa hii ya Serikali katika Halmashauri Kuu ya Taifa aliachiwa Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mheshimiwa Samuel Sitta. Baadaye, baada ya kikao nilimtafuta Ndugu Sitta, nikampa pole kwa kupewa jukumu la kueleza jambo ambalo halielezeki.
Tuwajali Mgambo
Mhariri,
Hoja yangu ni kuhusu Jeshi la Mgambo. Kauli ni jeshi la akiba. Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi bila majibu, kaulimbiu ni jeshi la akiba, lakini si kweli, bali ni jeshi la kutelekezwa na kukamuliwa. Haliendani na kaulimbiu.
Katiba ya nchi siyo ya CCM
Mhariri JAMHURI,
Nachukukua nafasi hii kwanza kulipongeza Gazeti la JAMHURI kwa kujitolea kuweka wazi kuhusu dawa za kulevya na pia kuhusu uwindaji haramu.
Chadema sasa wajiandaa kutumia nguvu Ukerewe
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, kimetamba kwamba kitatumia nguvu ya umma kuishinikiza Mahakama imtoe rumande Mbunge Salvatory Machemli. Mahakama ya Wilaya iliamuru Mbunge wa Ukerewe apewe adhabu ya kwenda jela siku 14 kuanzia Novemba 6 hadi 20, mwaka huu, kutokana na kudharau amri iliyomtaka ahudhurie mahakamani kusikiliza kesi ya uchochezi namba 19/2013 inayomkabili.