Category: Makala
FIKRA YA HEKIMA
Wabunge hawa hawatufai
Nianze kwa kuwapa pole mawaziri Shamshi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), Dk. Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi) na Dk. Mathayo David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi), waliopitiwa na rungu la Rais Jakaya Kikwete la kuvuliwa nyadhifa hizo, wiki iliyopita. Huo ndiyo uwajibikaji wa kisiasa.
MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE
Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (9)
Katika sehemu ya nane, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alisema Rais ndiye aliyekiri kosa la Zanzibar kuingia katika OIC na pili ndiye aliyelazimika kukiri kule Dodoma kwamba utaratibu wa kushughulikia hoja ya Utanganyika ulikosewa lakini mawaziri wake mara zote mbili walitulia tu nakumuacha Rais ndiye akiri kosa na kubeba lawama. Ifuatayo ni sehemu ya kitabu cha Mwalimu Nyerere alichokiandika mwaka 1994 cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania. Endelea…
Katiba ya nchi yetu, na utaratibu tunaojaribu kujenga, vinataka kuwa katika hali kama hiyo, Mawaziri ndiyo wawajibike, na hivyo kumlinda Rais, si Rais awajibike, na kuwalinda Mawaziri wake, na tena kwa kosa ambalo si lake. Watu walioshindwa uongozi Bungeni, hata tukafikishwa hapa tulipo leo, ni Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa CCM.
FASIHI FASAHA
Lissu ni malaika, waziri au mwanasiasa?
Ni takriban wiki tatu sasa tangu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kipate mtikisiko mkubwa, mithili ya pata shika na nguo kuchanika, baada ya Kamati Kuu (CC) ya chama hicho kuwavua nyadhifa zote viongozi wake watatu.
KONA YA AFYA
Sababu za kupungua nguvu za kiume -5
Wiki iliyopita, Dk. Khamisi Ibrahim Zephania alizungumzia kwa kina homoni ya kiume na umuhimu wake katika tendo la ndoa. Sasa endelea kumfuatilia zaidi…
Milima, mabonde ya Nelson Mandela
Mpigania haki za weusi na alama kuu ya udhalimu wa mfumo wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, Mzee Nelson Madiba Mandela, amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu, kutokana na maambukizo ya mapafu kushindwa kutengamaa.
Nyerere na Uhuru wa Tanganyika
Nazungumzia Uhuru wa Tanganyika. Sizungumziii Uhuru wa Tanzania Bara.
Majuzi niliona mabango yaliyosambazwa jijini Dar es Salaam. Mabango hayo yalisomeka “SHEREHE ZA MIAKA 52 YA UHURU WA TANZANIA BARA”.