JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Uchumi

Je, kufanya biashara ni kipaji?

Msomaji mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Jackson, alinitumia pongezi na kuniuliza swali hili: “Sanga, kwanini wataalamu mnasema biashara ni kipaji? Usemi huu una maana gani? Na mfano hai, tazama jamaa zetu Wahindi, kwa Watanzania angalia Kanda ya Kaskazini –  Wachagga; kwa Nyanda za Juu Kusini angalia Wakinga. Unasemaje hapo?”

Katika makala ya leo nitajikita kulijibu swali hili.


Bahati nzuri ni kwamba nimesoma Shahada ya Biashara nikiwa chuo kikuu na huu mjadala wa ikiwa biashara ni kipaji ama la ulikuwa ni sehemu ya ‘assignments’ zetu katika somo la Ujasiriamali (Entrepreneurship). Mjadala huu unapatikana katika kitu wanachokiita tetesi (myths) kuhusu ujasiriamali.

 

Dalili njema Nishati, Madini Tanzania

* Wizara yapeleka vijana 20 China, Brazil kusomea uzamili kuhusu mafuta, gesi

* Katibu Mkuu awaasa makubwa, asema nchi inawategemea warudi kuisaidia

Dalili njema zimeanza kuonekana katika Wizara ya Nishati na Madini Tanzania, baada ya vijana 20 wazawa kuchaguliwa kwenda China na Brazil kusomea shahada ya uzamili (masters) kuhusu fani za mafuta na gesi.

Hii ndiyo dawa ya kuepuka bomoabomoa

Katika miaka ya 1980, bendi moja ya muziki wa dansi hapa nchini ilitunga wimbo uliokuwa na kibwagizo cha “bomoa ee, bomoa ee, tutajenga kesho!”

Misitu inavyoinufaisha Nanjilinji ‘A’ (5)

Katika sehemu ya nne, Dk. Felician Kilahama alizungumzia kazi ya kutoa huduma bora za kijamii na kujenga miundombinu imara katika nchi yenye eneo kubwa. Alisema shughuli hiyo inahitaji ujasiri mkubwa na uzalendo wa hali ya juu. Sehemu hii ya tano na ya mwisho, Dk. Kilahama anatoa hitimisho.

MISITU & MAZINGIRA

Misitu inavyoinufaisha Nanjilinji ‘A’ (4)

Pongezi kwa wananchi wa Nanjilinji ‘A’

Kwa kuzingatia mafanikio yaliyopatikana katika Kijiji cha Nanjilinji ‘A’ na kwa kuelewa kuwa mafanikio hayo yametokana na wanakijiji kudhamiria kwa dhati kutumia rasilimali misitu inayopatikana ndani ya mipaka ya kijiji chao bila kushurutishwa na mtu yeyote, napenda nichukue fursa hii kutoa pongezi zangu za dhati kwa uongozi wa kijiji na wakazi wake wote kwa mafanikio hayo ya kutia moyo.

Tony: Nauza kahawa na digrii yangu

*Ni mhitimu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam

*Anauza kahawa stendi ya mabasi Ubungo

*Awaasa wasomi kutodharau kazi, aeleza mazito

Wakati vijana wengi waliohitimu elimu ya chuo kikuu wakikumbatia dhana ya kutarajia kuajiriwa serikalini na kwenye kampuni kubwa, hali ni tofauti kwa Tony Alfred Kirita, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).