Category: Uchumi
Mikopo ni sehemu ya biashara
Mikopo ni sehemu ya biashara. Huwezi kuanzisha biashara pasipo kukopa na huwezi kukua sana kibiashara pasipo mikopo.
Kila mtu ni mjasiriamali
Watu wengi huwa wananiuliza swali hili mara kwa mara, “Je, kila mtu ni lazima awe mjasiriamali?”
Nimekuwa nikiwajibu na leo ninataka kulijibu kwa namna nyingine na kwa upana. Ili kulijibu swali hili ninaomba nitumie Biblia kupata baadhi za rejea.
Kulalamika kunalowesha uchumi wetu
Naandika makala hii nikiwa nahudhuria kongamano la uwekezaji kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. Wiki zijazo nitawashirikisha fursa za kibiashara na kiuwekezaji zilizopo Nyanda za Juu Kusini (mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya).
Wajasiriamali na uchumi wa Afrika Mashariki
Leo ninapenda tuperuzi nafasi ya uelewa wetu sisi wajasiriamali na Watanzania kwa jumla, linapokuja suala la uchumi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Unapotaja Afrika Mashariki ni kwamba kuna mambo ya msingi yanayoushikilia uhusiano huu.
Pamoja na mambo mengine, nguzo kuu ya uwepo wa Jumuiya hii ni suala la uchumi. Ndiyo maana tunaongelea soko la pamoja, kuunganisha sarafu zetu, kusafiri kwa mitaji na rasilimali watu.
Puma yaihama Bandari Dar
Kampuni ya Mafuta ya Puma iko mbioni kuihama Bandari ya Dar es Salaam na kupitishia bidhaa zake katika Bandari ya Beira nchini Msumbiji.
Hatua hiyo ya Puma itazihusisha bidhaa za mafuta na vilainishi vinavyosafirishwa kwa ajili ya matumizi ya nchi za jirani.
Mtoa habari kutoka ndani ya kampuni hiyo aliieleza JAMHURI kwamba sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na mfumo usioridhisha uliopo katika Bandari ya Dar es Salaam katika ulipaji gharama za kuhifadhi mizigo na kodi.
Killagane: Gesi imekomboa uchumi Tanzania
*Gesi ya 25,000/- itatosha kupikia hadi maharage miezi mitatu
*Dar es Salaam, Mtwara wanufaika, magari 50 yatumia gesi
Ugunduzi wa gesi asilia kwa wastani wa futi za ujazo trilioni 46.5 ni ukombozi wa wazi kwa uchumi wa Tanzania. Thamani halisi inayokisiwa kwa gesi hii ni karibu dola bilioni 500 za Marekani, kiwango ambacho ni mara 50 ya uchumi wa sasa. Kati ya gesi hii iliyogunduliwa Kijiji cha Msimbati, mkoani Mtwara, na maeneo mengine ya nchi, futi za ujazo trilioni 38.5 zipo katika kina kirefu cha maji na futi za ujazo trilioni 8 zipo nchi kavu. Kuna dalili za mafuta, ila hayajagunduliwa. Katika makala haya, JAMHURI imehojiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Yona Killagane, ambaye anaeleza mambo mengi ya msingi yenye kutia matumaini kuwa sasa neema iliyokuwa ikisubiriwa hatimaye imewasili Tanzania. Endelea…