JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

Tunataka Katiba halisi  ya kudumu

Kama tujuavyo, hivi sasa Taifa letu liko katika mchakato wa kutafuta Katiba mpya ya nchi.

Katiba tunayotafuta sasa itakuwa nafasi ya katiba ya kudumu iliyoanza  kutumika mwaka 1977. Katiba ya nchi tunayotaka kuachana nayo imedumu kwa mbinde kwa sababu ina kasoro nyingi zilizoanza kupigiwa kelele tangu mwaka 1992, wakati Tanzania ilipoingia kwenye mfumo wa vyama vingi.

‘Privatus Karugendo anapotosha’

Privatus Karugendo, katika makala yake iliyochapishwa chini ya kichwa cha maneno, “Papa Benedict wa XVI Mfungwa wa imani anayetaka kuwa huru”, iliyoandikwa Februari 17, 2013, kurasa 11, 12 na 13, angeweka wazi kwamba Papa Benedict huyo aliwahi, kabla ya Aprili 5, 2009, kumvua madaraka ya shughuli za upadri, pengine nisingekuwa na hamu ya kuandika makala haya.

Udini sasa nongwa (1)

 

Siku za karibuni kuanzia wakati ule wa Sensa ya Watu na Makazi, neno UDINI limekua na linasikika mara kwa mara. Katika baadhi ya magazeti kama JAMHURI, kuna mfululizo wa makala za udini, mathalani makala za Ndugu Angalieni Mpendu – FASIHI FASAHA.

CCM irudishe mali za umma serikalini

Tanzania ilikuwa nchi inayofuata mfumo wa chama kimoja hadi mwaka 1992, wakati nchi wahisani za magharibi ziliposhinikiza nchi zote duniani zinazoendelea, kuanzisha mfumo wa vyama vingi kama ishara ya kujenga misingi bora ya demokrasia kwa jamii.

NUKUU ZA WIKI 68

Nyerere: Tunamtaka rais anayechukia rushwa

“Rushwa ni adui wa haki. Tunamtaka rais atakayelitambua hilo, atakayeichukia rushwa hata ukimuangalia aoneshe kweli anaichukia rushwa, sio rais anayesema kweli rushwa ni adui wa haki…. lakini ukimwangalia usoni unashangaa na kusema…. aaaah kweli huyu?”

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Waziri anapong’ang’ania wizara iliyomshinda

Dk. Shukuru Kawambwa ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Kwa kusema kweli hajafanya lolote zuri la kumsifia tangu alipoteuliwa kuwa waziri.