JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

Udini sasa nongwa (5)

Katika sehemu hii ya tano na ya mwisho, Brigedia Jenerali mstaafu Francis Mbenna, anahitimisha makala yake ya awali kuhusu udini na athari zake nchini Tanzania. Maudhui  kwenye makala haya ni kuwasihi Watanzania wote, bila kujali jinsi, hali, rangi na tofauti zozote zile, kuungana katika kukabiliana na hatari ya udini inayolinyemelea Taifa letu kwa kasi.

NuKUU ZA WIKI

  Nyerere: Wanadamu huongozwa na sheria “Nchi zote duniani huongozwa na wanadamu na si malaika. Wanadamu hawa huongozwa na Sheria na si kwa akili zao wenyewe.”   Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyasema haya wakati akihimiza Watanzania kulinda…

Siasa inavuruga masuala ya Taifa

Tunapozungumzia siasa hatuwezi kudai kwa haki kwamba siasa ni kitu kibaya. Ungeweza kusema kwamba siasa ni maneno mazuri yanayomtoa nyoka pangoni. Kwa kifupi siasa inasaidia kutatua matatizo.

Tuache kufyatua maneno – 2

 

Katika Kamusi hiyo, neno, ‘ari’ linaainishwa kuwa ni “hamu ya kutaka kukamilisha jambo na kutokubali kushindwa; ghaidhi, hima, nia, kusudio’. Hii ina maana kwamba matumizi ya neno ‘changamoto’ yameachanishwa na ufafanuzi wa Kiswahili.

Jukwaa la Wakristo limenishangaza

Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) linalojumuisha Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekosti Tanzania (PCT) na Kanisa la Waadventisti Wasabato (SDA), limenishangaza. Limenishangaza kwa lililolitoa hivi, kufuatia mkutano wake wa dharura uliofanyika Kurasini, Dar es Salaam, Machi 8 mwaka huu, ukiwahusisha maaskofu 117 wa makanisa mbalimbali nchini.

Udini sasa nongwa (3)

Zanzibari kuna waislamu wengi na wakristo wachache sana, lakini katika uteuzi mbalimbali imewahi au imepata kusikika jina la mkristo likiteuliwa? Wakristo wa kule si wanahaki zile zile za ubinadamu na za uraia? Mfumo upi hapo kandamizi -ule Mfumo Kristo unaoogopwa upande wa Bara kama kandamizi kwa dini ya kiislamu au Mfumo Islam unaokandamiza kila dini isipokuwa uislamu kule Zanzibar?