JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

Udini sasa nongwa (5)

Katika makala iliyopita kwenye safu hii, tuliandika kwa makosa kuwa makala ile ingekuwa hitimisho. Tena kukawa na kosa lililoonyesha kuwa ilikuwa sehemu ya tano. Usahihi ni kwamba hii ndiyo sehemu ya tano na ya mwisho katika mfululilo wa makala hii…

Tatizo la Serikali ni kufuga matatizo

Nikitaka kusema kweli (na ni lazima niseme kweli), Serikali ya Tanzania si mbaya kama watu wengine wanavyotaka kutuaminisha.

Alikuwa nani katika maisha ya Mwalimu Nyerere?

Siku moja niliulizwa ninamkumbukaje Mama Joan Wicken? Haraka haraka jibu lililonijia kichwani lilikuwa: “Alikuwa mchapa kazi hodari sana, aliyeitumikia nchi yetu kwa moyo wake wote na kwa nguvu zake zote!”

Mbatia jasiri wa kuigwa

 

Wahega walisema kwamba linaweza kutokea usilolitarajia kamwe. Sikutarajia hata siku moja kwamba Mbunge wa kuteuliwa na Rais atajiingiza kwa kishindo katika historia ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutenda kinachofanana na kuuma mkono unaomlisha, nia yake ikiwa kujiepusha na mgongano wa maslahi.

NUKUU ZA WIKI

Nyerere: Kubaguana kutavunja Taifa

“Tabia hii ya kubaguana ambayo inafanana na ile ya Uzanzibari na Utanganyika, itavunja Taifa siku moja. Dhambi ya ubaguzi haiishi hata siku moja.”

 

Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyasema haya kukemea ubaguzi wa kikabila, ukanda, udini na rangi nchini. Alizaliwa Arili 13, 1922, alifariki Oktoba 14, 1999.

Matumaini aliyoleta Kinana yamepotea

Kwa muda mrefu wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikuwa wamekata tamaa na chama chao. Walikuwa na hakika kwamba chama chao kingeangushwa  katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Kwa nini!