Category: Siasa
KONA YA AFYA
Vidonda vya tumbo na hatari zake (10)
Wiki iliyopita, Dk. Khamis Zephania alielezea dalili za vidonda vya tumbo yakiwamo maumivu na tofauti yake kulingana na rika. Sasa endelea kumfuatilia katika sehemu hii ya kumi…
KAULI ZA WASOMAJI
Askari GGM wanatumaliza
Viongozi wa Wilaya ya Geita wajue kuwa askari maarufu kama ambush na wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) wanatutesa sana, baadhi yetu wanafanywa vilema na wengine wanauawa. Wapo watu wengi wamekufa kutokana na kupigwa risasi. JAMHURI tusaidieni kupigia kelele tatizo hili, tunakwisha!
Paulo, Geita
0758 479 354
Watanzania tukazane kuwekeza kwenye ardhi
Leo ni mwaka mmoja kamili umepita tangu nilipoandika makala hapa safuni yaliyokuwa na kichwa, “Njooni shambani mtajirike”. Ilikuwa ni makala yaliyotoa shime kwa Watanzania kuchangamkia fursa ya uwekezaji kwenye kilimo cha miti.
NUKUU ZA WIKI
Julius Nyerere: Kumteta mtu ni kumdhuru
“Wengine humwona mwenzao anafanya kosa, badala ya kumwambia pale pale kijamaa kwamba atendalo ni kosa, watanyamaza kimya. Lakini hawanyamazi kabisa! Watakwenda kumteta katika vikundi vya siri siri. Mateto haya si ya kumsaidia mwenzao, ni ya kumdhuru.”
Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Ndiye Rais wa Kwanza wa Tanganyika na baadaye Tanzania.
Tumetoka wapi, tupo wapi, tunakwenda wapi
Hotuba ya Mwalimu Julius K. Nyerere Aliyoitoa Wakati wa Kilele cha
Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani, Mbeya, Mei Mosi, 1995.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alialikwa kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika kitaifa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Mei Mosi, 1995. Katika hotuba yake, Mwalimu alielezea historia ya vyama vya wafanyakazi duniani. Aidha, alitumia fursa hiyo kutoa maoni yake kuhusu hali ya kisiasa na kiuchumi nchini pamoja na ushauri kuhusu mambo wananchi wanayopaswa kuzingatia wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huo, hasa sifa za wagombea nafasi za uongozi kuwa ni pamoja na kila mmoja kujiuliza ataifanyia nini nchi yake baada ya kuchaguliwa, na anakwenda kufanya nini Ikulu. Ifuatayo ni hotuba ya Mwalimu…
Navumilia kuwa Mtanzania
Tanzania ni nchi yangu ninayoipenda kwa moyo wote, ni kisiwa cha amani, upendo na utulivu, ni nchi yenye watu wakarimu na wenye upendo na mahaba yasiyopimika. Watanzania wanaishi kwa kupendana kuthaminiana na kuheshimiana bila kujali matatizo au changamoto zinazowakabili, kila mmoja akimuita mwenzake ndugu.