JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

Tuepuke vurugu kwa kutenda haki

Juma lililopita, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe,  alimwomba Rais Jakaya Kikwete auridhie Muswada wa Marekebisho ya Mabadiliko ya Sheria ya Katiba, kwa lengo la kuepusha vurugu nchini.

Wadau wasikitika magazeti kufungiwa

Wadau mbalimbali wa habari wameeleza kusikitishwa kwao na kufungiwa kwa magazeti ya Mwananchi na Mtanzania.

Gazeti la Mwananchi limefungiwa kwa siku 14 wakati Mtanzania  limefungiwa kwa siku 90.

Tanzania tuige Bunge la Kenya

Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama nchini Kenya imeonesha mfano mzuri unaostahili kuigwa hapa Tanzania. Kamati hiyo imetangaza kusudia lake la kuwahoji wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa Kenya kuhusu tukio la ugaidi katika jengo la kitega uchumi, Westgate jijini Nairobi.

Utapeli udhibitiwe Tanzania

Maoni ya Mhariri wa JAMHURI wiki iliyopita, yalipendekeza mtandao wa utapeli wa madini uliopo hapa nchini uvunjwe kwa sababu unaathiri uchumi, heshima na sifa ya Watanzania mbele ya uso wa Dunia. Kwamba watoto na wajukuu wao watakosa wa kufanya naye biashara, hivyo Taifa letu kuendelea kuwa tegemezi.

Tunataka viongozi kama Mwalimu Nyerere

 

Ndugu Mhariri,

 

Siasa ni mfumo wa utawala wenye kuleta ustawi wa nchi kimaendeleo, utumikao duniani kote. Mfumo huu umejengeka kwa misingi yake kutokana na kubeba mhimili mkubwa wa nchi au taifa lolote.

 

 

Yah: Chondechonde kumbukeni Bunge la Karimjee, Dar es Salaam

Nashukuru kwa kuwa Bunge letu sisi lilikuwa pale Dar es Salaam, Karimjee na pia hakuna vikinga hatari kama vilivyopo katika Bunge lenu la pale Dodoma, na wakati ule idadi ya wabunge ilikuwa ndogo, kiasi cha 72 tu, waliochaguliwa kwa jembe na nyumba.