Category: Siasa
Chakula cha bure: Falsafa ya Pinda!
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha inaisimamia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ili igawe chakula cha bure kwa kaya 20,000 zinazoishi katika Tarafa ya Ngorongoro.
Vijana na makundi matatu ya uongozi
Mwaka 1974 hadi 1978 nilikuwa Katibu Mkuu wa kwanza miongoni mwa waasisi wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA), Dar es Salaam. Mwaka 1976 Katibu wa wanachuo, Chuo cha TANU Kivukoni, na Katibu wa TANU (Radio Tanzania Dar es Salaam-RTD) kazini.
Kijiji chachomwa kumpisha Mzungu
*Uamuzi wa Mahakama ya Rufaa wapuuzwa na viongozi
*Wanaopinga kuhama wabambikiwa kesi mahakamani
*Mwanamke afungwa miezi 6 jela, mtoto alelewa na bibi
Wananchi kadhaa katika eneo la Maramboi, Kijiji cha Vilima Vitatu, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, hawana makazi baada ya nyumba zao kuchomwa moto ili kumpisha mwekezaji raia wa Ufaransa.
MATHIAS CHIKAWE: Mwanasheria aliyejifunika siasa
* Asema yeye kuwa Waziri wa Katiba na Sheria anajiona kama samaki aliyetumbukizwa majini
Wakazi wa Jimbo la Nachingwea mkoani Lindi, wana kila sababu ya kujivunia bahati ya wabunge wao kuteuliwa na Rais kuongoza wizara mbalimbali hapa Tanzania. Edgar Maokola-Majogo, aliyeliongoza jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 30, pamoja na wizara nyingine, alipata kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, kitengo cha Kupunguza Umaskini na Kuratibu Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Waziri wa Nishati na Madini.