JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

FIKRA YA HEKIMA

Bravo Kikwete, lakini agizo lako lisilenge mahindi, Njombe pekee

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete, anastahili pongezi kutokana na hatua yake ya kutengua msimamo wa muda mrefu wa Serikali kuwazuia wakulima kuuza mahindi nje ya nchi.

FASIHI FASAHA

Vyama vya upinzani bado ni vichanga? (1)

Mara kwa mara Watanzania huzungumzia juu ya vyama vya siasa, hasa vyama wanavyoviita vyama vya upinzani au vya ukingani. Mazungumzo hayo ni kuhusu sababu za kuanzishwa, shughuli zinazofanywa na malengo ya vyama hivyo.

Serikali isisaidie shule za watu binafsi

Wazo limetolewa la kuitaka Serikali isaidie shule za watu binafsi na tayari wazo hilo limeanza kupigiwa debe serikalini.

Taarifa rasmi ya Kambi ya Wanyamapoli bungeni

 

Mheshimiwa Spika, awali ya yote tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa Bunge lako tukufu kwa kutambua uwepo wetu hapa bungeni leo hii.

NUKUU ZA WIKI

 

Nyerere: Ole wao wale watakaoifanya  siku hiyo  isiepukike

Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku hiyo!

Na ole wao wale watakaoifanya siku hiyo isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe haitofika.

Kauli hii ilitolewa na Hayati baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Januari 1966

MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE

Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (3)

Huu ni mtiririko wa maandishi yaliyo katika kitabu cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania kilichoandikwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwaka 1994. Sehemu iliyopita Mwalimu alieleza kuzuka kwa suala la Zanzibar kujiunga OIC, na viongozi wakaliombea bungeni mwaka mmoja wa kulitafakari. Endelea…

BUTIAMA 2: 8:1993

Masuala mawili hayo, (i) msimamo wa Zanzibar kuhusu utaratibu wa kuchagua Makamu wa Jamhuri ya Muungano, na (ii) Zanzibar kuingia katika OIC ndiyo yaliyokuwa sababu ya ujumbe wa mara kwa mara kati yangu na Rais wa Jamhuri ya Muungano; na ndiyo Rais na mimi tulikuwa tukiyazungumza Butiama, tarehe 2 Agosti, 1993. Baada ya kuyazungurnza kwa muda mrefu na kuelewana nini la kufanya, Rais akanifahamisha kwamba Waziri Mkuu kamletea habari kwamba: