Category: Siasa
Yah: Sasa ni mwendo wa msoto kutafuta kula, si kura
Najuta kuzaliwa maskini na katika familia ya ukulima, ningelipenda nizaliwe katika familia ya uanasiasa au ufanyabiashara, na kuwa na nafasi ya kuweza kuwa na maisha bora kama ilivyo kwa familia hizo nyingi pasi na familia zetu za wakulima. Napenda kuwa …
Msumbiji, Tanzania tuenzi undugu wetu
Msumbiji na Tanzania, ukweli ni nchi ndugu tangu zama. Msumbiji tangu hizo zama ni sumbiji. Tanzania ni nchi mpya iliyoundwa kutokana na nchi mbili huru, Tanganyika na Zanzibar. Katika ukweli huo nchi hizo ndizo hasa ndugu wa Msumbiji. Ndipo ninapothubutu…
Raia kukataa kukamatwa taratibu zikikiukwa
Siku zote wananchi wamekuwa wakililalamikia Jeshi la Polisi kwa namna linavyoendesha shughuli zake hasa wakati wa ukamataji (arresting). Matumizi ya nguvu, ubabe na kutofuata sheria na utaratibu maalum vimekuwa ndiyo tatizo kubwa kwa wananchi dhidi ya askari. Siyo siri, askari…
Dhana ya Demokrasia yetu inakumbana na changamoto
Pamoja na hatua zilizofikiwa kukuza demokrasia chini ya mfumo wa vyama vingi vya siasa, bado ziko changamoto zinazoathiri hali ya kukua na kushamiri kwa demokrasia nchini. Ile tafsiri asilia ya demokrasia inasema hivi: Serikali inayoongozwa na watu. Aidha ni aina…
Nenda Sophia Yamola, nenda mpekenyuzi ukidai haki yako
Katika kipindi cha wiki moja, tasnia ya habari imepata pigo kubwa kwa kuwapoteza wapiganaji wake wawilikatika tasnia hii. Kwanza alikuwa ni Samwel Chamulomo, aliyekuwa Mtangazaji wa TBC Kanda ya Kati, mauti yalipomkuta akiwa mkoani Dodoma. Pili ni Sophia Yamola, mwandishi…
Tumelogwa kuwa wanafiki
Awamu ya kwanza ya harambee ya ujenzi wa kituo cha yatima, shule ya sekondari na msikiti Patandi, Arumeru mkoani Arusha, imefana kwa kiwango kikubwa na kuwa miongoni mwa vielelezo muhimu vya kuuendeleza umoja na mshikamano wa Watanzania bila ya kujali…