Category: Siasa
Denis Vedasto: Mjasiriamali aliyekuta na JK
“Niliona ni vyema nikuze kipaji changu kuliko kitumike na watu wengine kwa kuajiriwa, kwani nina ubunifu mkubwa kuliko ndiyo maana niliona ni bora nianzishe kampuni yangu.” Hayo ni maneno ya Denis Vedasto, mkazi wa Kitunda, Dar es Salaam ambaye ni mjasiriamali anayejishughulisha na utengenezaji wa vitanda vya hospitali, ambavyo vingine hutumiwa wakati wa kinamama kujifungua.
Dk. Lwaitama: Tuboreshe, tusivunje Muungano
Nimesikitishwa na aina ya uandishi wa habari uliojiweka wazi katika taarifa iliyonukuliwa kuandikwa na mwandishi wa gazeti moja la kila siku (Tanzania Daima la Agosti 7, 2012), Datus Boniface. Huyu mwandishi, pamoja na wahariri wake walioruhusu habari hiyo kuchapwa walithubutu kusema uongo kuwa eti “ Dk Lwaitama, Prof. Sheriff na Prof Shivji waliushambulia Muungano.” Tena, mwandishi huyu na wahariri walioruhusu habari hiyo ichapishwe wakaenda mbali zaidi na kutumia kichwa cha habari kilichosema eti ‘Shivji, Lwaitama wataka Muungano uvunjwe’.
Mjue Kada wa CCM Mohsin Abdallah
*Tume ya Jaji Warioba ilianika madudu yake
*Ni bilionea anayehodhi vitalu vya uwindaji
Hivi karibuni, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) aliuibua bungeni mkataba ulioingiwa baina ya kampuni za Uranium Resources PLC, Western Metals Limited na Game Frontiers of Tanzania Limited uliotengenezwa na Kampuni ya Kitanzania ya Rex Attorneys, na kusainiwa Machi 23, 2007.
Nyerere: Wazanzibari waamue
“Ikiwa Wazanzibari wataukataa Muungano, bila mashinikizo kutoka mataifa ya nje, siwezi kuwapiga mabomu kuwalazimisha.”
Haya ni maneno ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kueleza nia yake ya wazi kuwa ikiwa Wazanzibari wanaona hawautaki Muungano hawezi kuwazuia.
Biashara za sasa zinahitaji u-sasa
Ingawa kuna mambo mengi hapa katika u-kisasa, kwa leo nitagusia maeneo matatu tu. Mosi, kuweka biashara katika mifumo rasmi; pili kuwa na maono; na tatu kutengeneza mfumo wa kurithisha biashara kutoka baba kwenda kwa watoto – kutoka kwa wajukuu kwenda kizazi cha pili. Biashara katika mifumo rasmi ina dhana pana, lakini kwa urahisi kabisa ni kuendesha biashara katika mifumo inayoelezeka. Ni ile hali ambayo mmiliki unapokuwapo au kutokuwapo biashara inaendelea kama kawaida.
Hotuba iliyowazima wabunge mafisad
Bunge linanuka rushwa. Baadhi ya wabunge wanapokea rushwa ili kutetea maslahi ya wanaowatuma. Lakini wapo wabunge jasiri walioamua kupambana na wenzao wala rushwa kama inavyothibitishwa na Hotuba ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Wizara ya Nishati na Madini,…