JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

Siri zaanza kuvuja rushwa Kamati za Bunge

 

Mtandao wa wafanyabiashara wahusishwa

Kamati ya Maliasili, Mazingira yaguswa

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira aliyejitambulisha kuwa ni mpinga vitendo vya rushwa, ameamua kuandika makala hii kueleza baadhi ya vitendo vya rushwa ndani ya Kamati hiyo. Hii ni sehemu ya makala ya mbunge huyo ambaye kwa sasa tunalihifadhi jina lake.

UTANGULIZI

Tarehe 28 Julai 2012, Bunge la Tanzania liliingia katika historia baada ya Spika Anne Makinda kutangaza kuivunja Kamati ya Nishati na Madini pamoja na kamati nyingine zinazotuhumiwa kwa rushwa.

Spika alifikia hatua hiyo baada ya kuwapo kwa harakati za wafanyabiashara wa sekta ya mafuta kufanya mipango kwa zaidi ya wiki mbili za kuwashawishi wabunge washinikishe kujiuzulu kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, na Katibu Mkuu Eliakim Maswi kwa kile kinachodaiwa kutoa zabuni kwa kampuni ya Puma Energy ya kuiuzia mafuta Tanesco kwa ajili ya mitambo ya umeme wa dharura ya  IPTL. Harakati zililenga wabunge wengi wenye ushawishi bungeni, wakianzia na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya

Kikwete: Hakuna vita

“Namhakikisha ndugu yangu, watu wote wa Malawi kwamba hatuna nia wala mpango wa kuingia vitani. Hatuna matayarisho ya Jeshi wala jeshi halijasogea popote… mimi ndiye kamanda mkuu wa jeshi na sijapanga wala kutoa maelekezo ya vita.”   Haya ni maneno…

Je, wote tuwe wajasiriamali?

Nianze kwa kushukuru na kutambua mirejesho ya wasomaji wa safu hii ambao wanaongezeka kila wiki. Mirejesho mnayoniletea kwa ujumbe mfupi wa maandishi, kupiga simu na kuniandikia baruapepe ina thamani na umuhimu mkubwa sana katika kunogesha safu hii.

Bunge la sasa linaelekea wapi? (2)

Duniani kote upinzani huwa una tabia ya kuchokonoa upungufu wa hoja na kisha kuonyesha vipi maboresho yangekuja kama wao wangeongoza Serikali. Hii maana yake bungeni unakuwapo ukosoaji wa aina mbili.

Kennedy: Tusiichekee vita

“Mwanadamu anapaswa kumaliza vita, vinginevyo vita itammaliza mwanadamu.”

Haya ni maneno ya Rais wa 35 wa Marekani aliyeuawa mwaka 1963. John F. Kenney alikuwa akiamini kuwa dunia inaweza kuwa salama zaidi kwa kutoendekeza vita.

Barua ya kibiashara kwa BRELA

Baada ya kuandika makala ya “Biashara za sasa zinahitaji u-sasa”, kuna jambo nililitazamia ambalo limetokea kama yalivyokuwa matarajio yangu. Kumekuwa na wasomaji wengi nchi nzima ambao wameleta maombi na ushauri wakitaka niwasaidie kusajili biashara zao katika mfumo wa kampuni.