JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

Kikwete polisi wanaanza kuyeyusha heshima uliyojijengea

Mwaka 2008 nilibahatika kuwa mmoja wa watu waliopata fursa ya kusafiri na Rais Jakaya Kikwete kwenda jijini Washington, Marekani. Safari hii ilikuwa ikihusiana na mambo mbalimbali lakini kubwa ni kushawishi Serikali ya Marekani kuridhia Mpango wa Millennia Challenge Cooperation (Account) – MCC.

Waziri Mgimwa ahimiza ufanisi PPF

Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, amehimiza utendani makini utakaongeza ufanisi katika Mfuko wa Pensheni za Mashirika ya Umma (PPF) nchini.

Elimu ya Tanzania vipi?

Baada ya matokeo ya mitihani ya darasa la VII ya mwaka 2011 kutangazwa, kumetokea tashtiti kubwa katika nchi hii. Kule kutangazwa kwamba wanafunzi 5,200 hawajui kusoma wala kuandika, lakini wamo miongoni mwa watoto 567,567 waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka huu, kumewashangaza wengi. Naona kama ni jambo fulani la kisanii!

Mandela: Urafiki na adui yako

“Ikiwa unataka kupata amani na adui yako, unapaswa kufanya kazi na adui yako, kisha anageuka na kuwa mdau wako.” Haya ni maneno ya Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela aliyemaliza vita ya ubaguzi wa rangi kwa kutumia mfumo…

Mgogoro wa Tanzania, Malawi ngoma mbichi

*Malawi waendelea kukomaa wachukue ziwa lote

*Tanzania yasema mgawo ni nusu kwa nusu tu

*Wazee wa hekima Afrika kuitwa kusuluhisha

*Wasipoafikiana kutinga Mahakama ya ICJ

*Yote hayo yakishindikana JWTZ wataamua

 

Kumekuwapo desturi ya wanasiasa kutafuta jambo la kuwawezesha kuwajenga kisiasa, ili waweze kushinda uchaguzi, hasa Uchaguzi Mkuu. Mzozo wa mpaka wa Ziwa Nyasa unaozihusisha nchi za Tanzania na Malawi unatajwa kuwamo mwenye mtiririko huo wa kidesturi. Malawi inatarajia kuingia kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2014, hivyo kete inayotumiwa na chama cha Rais Joyce Banda, pamoja na vyama vingine vya siasa ni kutaka kutunisha msuli kupitia mzozo wa mpaka kati yao na Tanzania kwa lengo la kujipa kuungwa mkono na Wamalawi wengi.

Bunge la sasa linaelekea wapi? (3)

Kwa namna mwenendo unavyoonekana katika Bunge, nashauri waheshimiwa wabunge wauzibe ule ufa namba tatu, ulioelezwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, unaotikisa Taifa letu. Ufa huo ni ule wa “Kuendesha mambo bila kujali sheria (Nyufa: uk. 14 ibara ya pili)”