Category: Siasa
Mramba: Kuleni nyasi
“Tupo tayari kula hata nyasi, lakini lazima ndege ya Rais inunuliwe”
Haya ni maneno aliyoyatoa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Pesambili Mramba wakati wa Awamu ya Tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa Bunge lilipoelekea kukataa ununuzi wa ndege ya Rais.
Tujifunze kutokuwa wavivu wa kufikiri
Mwalimu Julius Nyerere katika kitabu chake cha TUJISAHIHISHE alisema, “Wengine humwona mwenzao anafanya kosa, badala ya kumwabia pale pale kijamaa kwamba atendalo ni kosa, watanyamaza kimya. Lakini hawanyamazi kabisa! Watakwenda kumteta katika vikundi vya siri siri.
Nani anawashika mkono wajasiriamali?
Mwezi mmoja uliopita niliandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari “Barua ya biashara kwa BRELA”. Brela ni Mamlaka ya Uandikishaji Biashara na Leseni. Baada ya kuitoa gazetini niliituma pia barua hiyo huko Brela kwa njia ya barua pepe.
TAFAKURI YA HEKIMA
Polisi wangeweza kuepusha mauaji ya Mwangosi
Nianze kwa kutoa salamu za rambirambi na pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na watu wote walioguswa na kifo cha mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, amina.
Wafadhili wa migogoro Loliondo wajulikana
Suala la mgogoro wa Loliondo limekuwa likitawala katika vyombo vya habari kwa miongo kadhaa sasa. Safari hii kuna kampeni inayoendeshwa kwenye mtandao kwa wiki kadhaa sasa. Chanzo cha mjadala huo ni kwamba Serikali ya Tanzania inataka kuwaondoa wafugaji wa Kimasai ndani ya Loliondo ili kupisha biashara ya uwindaji wa kitalii. Kampeni hiyo inaendeshwa na mtandao wa Avaaz.
China yaipatia Zanzibar mabilioni
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China zimetiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kiufundi ambako Zanzibar itapatiwa Sh bilioni 14.8.