JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: JAMHURI YA WAUNGWANA

Sijajua Watanzania tunachotaka

Mwalimu Julius Nyerere aliamini katika dhana ya maendeleo ya watu, na si maendeleo ya vitu. Dhana hii imepewa tafsiri nyingi. Wapo wanaoamini kuwa Mwalimu hakutaka kuona barabara, majengo makubwa makubwa na miradi mingine yenye thamani ya mabilioni ya fedha. Lakini…

Kwa hili RC Chalamila amepatia

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, huwa hakosi vituko! Wengi wetu tulitarajia wiki iliyopita afungue mwaka mpya wa 2020 kwa kituko! Hakufanya hivyo! Badala yake ameukaribisha mwaka kwa kutoa maelekezo mazuri yanayopaswa kuungwa mkono, si Mbeya pekee, bali nchini…

Staili ya zimamoto inaua elimu

Jamii au familia makini ni ile inayoweza kwa akili za kibinadamu kutabiri na kuweka mipango kutokana na kinachotarajiwa. Kwenye ngazi ya familia yapo yanayopaswa kufanywa na wazazi ili kukabiliana na makusudio au mipango yao ya kupanua familia. Vivyo hivyo, serikali…

Tujipendekeze kwa kiasi

Awali ya yote niwaombe radhi wapendwa wasomaji kwa kuwatupa mkono kwa kipindi kirefu sasa. Kwa siku za karibuni nimekuwa na dhima nyingi, kiasi cha kujikuta nikishindwa kutimiza yote niliyokusudia kwa wakati mmoja. Itoshe tu kuwashukuru mno kwa kuendelea kwenu kuwa…

Miaka minne kazi bado kubwa

Tarehe ya leo miaka minne iliyopita, Dk. John Magufuli, aliapishwa kuwa Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuapishwa kwake kulimpa muda wa kuandaa dira yenye kuonyesha mwelekeo wa aina ya serikali anayokusudia kuiunda kwa ajili ya kutekeleza…

Polisi acheni wapinzani wapumue

Kila mara niwazapo hatima ya umoja na mshikamano wetu huwa ninapekua na kusoma kijitabu kidogo, lakini kilichoshiba maneno ya busara sana kinachoitwa ‘Tujisahihishe’. Kiliandikwa na Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 1962. Ni bahati tu kuwa sina mamlaka ya kuamuru, vinginevyo ningeamuru…