JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: JAMHURI YA WAUNGWANA

Tumefeli somo la ustaarabu

Kuna ‘kosa’ nimelitenda hivi karibuni. Kosa lenyewe ni la kuwakwida vijana wawili walioamua-bila soni- kujisaidia hadharani katika barabara tunayoitumia mtaani kwetu. Wale vijana sura zao zilikuwa ngeni kwangu. Nilipowakaribia, nilishuka katika gari na kuwauliza kwanini wameamua kujisaidia hadharani. Jibu lao…

Video iliyonitoa machozi

Muda ni saa 3:35 usiku wa Ijumaa ya wiki iliyopita. Nimejipumzisha barazani baada ya kupambana na foleni za Dar es Salaam. Simu yangu inaashia kuingia kwa ujumbe wa WhatsApp. Nafungua na kuanza kuusoma: “Kuna njia gani ya kuwapata hawa wanaume…

Bado sijaona kosa la Rais Magufuli

Tukisema tunaambiwa mahaba yametuzidi. Tunaambiwa tunyamaze kwa kuwa furaha yetu ni ya muda- bado yuko kwenye honeymoon (fungate). Wapo wanaosema eti hata Jakaya Kikwete, alipoingia madarakani mwaka 2005 tulimshangilia, lakini baadaye ni sisi hao hao tuliogeuka na kuanza kumlaumu kwa…

Rais Magufuli angazia mafuta ya mawese (2)

Wabunge wazoefu wamelia na kuiomba Serikali isibariki “mauaji” haya kwa wakulima wetu. Wametumia kila aina ya maneno kuwashawishi wakubwa serikalini, lakini mwishowe wameshindwa. Historia itawahukumu kwa haki. Hansard zipo. Nani hawezi kuamini kuwa ushindi ambao serikali imeibuka nao bungeni umetokana…

Wachuuzi wakiachwa hivi hivi ni ‘jeshi hatari’

Juzi nilishiriki mjadala mfupi katika mtandao wa kijamii wa Facebook. Niliweka picha ya wachuuzi waliovamia eneo la waenda kwa miguu katika eneo la Ubungo, Dar es Salaam. Maudhui ya picha hiyo yalikuwa kuwafikishia taarifa (kana kwamba hawazioni wala hawazijui) viongozi…

Hili si shamba la bibi aliyekufa

Nimepata kuifananisha hali ya sasa ya mapambano ya kuijenga nchi yetu na ile ya nchi iliyo vitani. Taifa linapokuwa vitani, hasa vita hiyo inapokuwa halali, wananchi wazalendo huungana kuitetea nchi yao isitwaliwe na adui. Kwa wazalendo, ushindi ndiyo dhima yao…