Category: Maoni ya Mhariri
Sumatra na porojo za kujikosha
Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) inapendekeza kuwapo kwa kanuni kadhaa zinazolenga kupunguza ajali nchini. Katika mapendekezo hayo, Sumatra wanataka umri wa madereva wa magari ya abiria uwe kati ya miaka 30 hadi 60. Wamejikita kwenye hoja hiyo dhaifu kwa imani kwamba vijana chini ya umri wa miaka 30 ndiyo chanzo kikuu cha ajali za mabasi nchini!
Bila kuheshimu Katiba tutayumba
Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwapo mjadala mkali kuhusu uhalali wa baadhi ya majaji na sifa zao za kuifanya kazi hiyo. Kumekuwapo madai kwamba baadhi ya majaji wameteuliwa ilhali wakiwa na rekodi mbaya za uombaji rushwa, uonevu, upendeleo na kukosa uadilifu.
Serikali iwanusuru mabalozi wetu
Katika toleo la leo tumechapisha taarifa zenye kuonyesha kuwa hali ya kifedha ya Balozi za Tanzania nje ya nchi ni mbaya. Habari hizi zinaonyesha kuwa Balozi karibu zote zinakabiliwa na madeni, zimekatiwa huduma za simu, maji, umeme na mifumo ya…
Madai ya Tundu Lissu yachunguzwe
Katika gazeti la leo kuanzia ukurasa wa kwanza tumechapisha ripoti maalum yenye kuonyesha hali ya wasiwasi katika muhimili wa tatu wa dola uliokasimiwa jukumu la msingi la kutoa haki. Wasiwasi huu umeibuliwa na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu kwa Kamati ya Uongozi ya Bunge.
Chonde chonde Malawi, ninyi ni ndugu zetu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ametangaza msimamo wa Tanzania kuhusu mgogoro wa mpaka kati ya Taifa letu na Malawi. Kwa mara nyingine, Serikali kupitia kwa Membe imeitaka Malawi, kampuni na makundi mengine, kuacha mara moja kuendelea na shughuli za utafiti wa mafuta na gesi katika Ziwa Nyasa. Kama alivyosema, Malawi wanadai kwamba mpaka wa haki kati ya Tanzania na Malawi ni pwani ya ziwa hilo kwa upande wa Tanzania.
Haya ndiyo mambo murua yanayoliliwa na Watanzania
Wizara ya Nishati na Madini imetangaza kupunguza gharama za kuunganishia wateja wake umeme. Gharama hizo zimepungua kwa wastani wa asilimia 30 na 77. Uamuzi huo ulitangazwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, bungeni mwishoni mwa wiki.