JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Maoni ya Mhariri

Nishati na Madini ni Mfano  wa kuigwa

 

Mwishoni mwa wiki iliyopita Wizara ya Nishati na Madini iilitoa taarifa ya utekelezaji wa kipindi cha miezi mitatu iliyopita chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BNR).

Hakimu huyu ashughulikiwe

Katika toleo la leo tumechapisha habari za kusikitisha juu ya matumizi mabaya ya madaraka katika Idara ya Mahakama Tanzania. Tumechapisha habari kuwa mtuhumiwa mwenye asili ya China alikamatwa Alhamisi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akiwa na madini ya tanzanite yenye thamani karibu Sh milioni 200.

Mwalimu asienziwe kwa porojo

Miaka 14 imeshatimia tangu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alipofariki dunia katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas jijini London, Uingereza, Oktoba 14, 1999.

Tuwe makini, mitandao ya uhalifu inaongezeka

Kwa muda sisi JAMHURI tumekuwa tukiandika habari zinazohusu wasafishaji na wauza mihadarati; na pia matapeli wa biashara ya madini waliokubuhu. Tulichobaini ni kwamba wahusika wakuu kwenye biashara, hii wanalindwa na baadhi ya viongozi wakubwa katika nchi yetu. Mitandao ya uhalifu katika Tanzania ni mipana na yenye nguvu kuanzia ngazi za chini hadi katika vyombo vya ulinzi na usalama.

Serikali isikilize kilio cha Waislamu

Septemba 23, mwaka huu Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu Tanzania wamemwandikia barua Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa kupinga utaratibu mpya wa mitihani na upangaji madaraja kuhusu masomo ya dini ya Kiislamu, kompyuta, lugha za Kiarabu, Bible Knowledge na Kifaransa. Masomo haya sasa yamegeuzwa ya hiari.

CAG awahishe ukaguzi Bukoba

Katika toleo la leo tumechapisha habari za mgogoro unaoendelea kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba. Mgogoro huu ni mkubwa kwa kiwango ambacho wananchi, watendaji, viongozi, wafanyabiashara na hata wanasiasa wamefika mahala hawaaminiani. Kila kona ya Bukoba kuna mazungumzo kwenye makundi.