Category: Maoni ya Mhariri
Hii ni aibu rushwa kukwamisha stendi
Habari tuliyoipa umuhimu wa pekee kwenye toleo hili inahusu mkwamo wa ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi ya mikoani eneo la Mbezi Luis, Dar es Salaam. Tumeeleza namna vitendo vya rushwa vinavyotishia mradi huo mkubwa kwenye sekta ya usafiri…
Hongera Wizara ya Kilimo, hongereni wapambanaji
Wizara ya Kilimo imezuia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) iliyopo Makutupora, Dodoma kuendelea na utafiti wa mbegu za GMO. Uamuzi huo ni majibu kwa kilio cha wazalendo waliojitokeza kupaza sauti kuhoji uhalali wa chepuo linalopigwa ili kuruhusu mbegu hizo…
Uonevu kwa wakulima ufikie tamati
Tunapongeza hatua iliyochukuliwa na serikali kwa wakulima wa korosho. Japo matokeo ya uamuzi huo hayajajulikana, lililo la msingi ni kuwa serikali imeonyesha kuwajali wananchi hao. Historia inaonyesha kuwa kwa miongo mingi wakulima wa mazao ya aina zote wamekuwa wakidhulumiwa licha…
Hongera Rais Magufuli
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli imetimiza miaka mitatu tangu ilipoingia madarakani mwaka 2015. Rais Magufuli alishika uongozi nchi ikiwa inakabiliwa na matatizo mengi ya kiuchumi, kijamii na kimaadili. Hatuna kipimo sahihi cha kubainisha kazi zilizokwisha…
Hongera RC Mtaka
Mkuu wa Mkoa (RC) wa Simiyu, Anthony Mtaka, ametoa msimamo wa namna alivyodhamiria kuubadilisha mkoa huo ili uendane na ‘Tanzania ya Viwanda.’ Kabla na baada ya kusifiwa na Rais John Magufuli, aliyemtaja kama RC bora nchini, Mtaka ameendelea kuonyesha maono…
IGP Sirro: Kuna urasimu mkubwa umiliki wa silaha
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP) Simon Sirro, ametoa mwito kwa wananchi wenye kustahili kuwa na silaha kuomba wamilikishwe ili wajilinde dhidi ya wahalifu. IGP Sirro alitoa kauli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari, ambapo pamoja na mambo…